LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 2, 2021

UWT DAR YAANZA MAADHIMISHO YA KUZALIWA JUMUIYA HIYO KWA KUTIA MKAZO SUALA LA MIKOPO KWA WANAWAKE, KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akikagua bidhaa za vyungu wakati akifungua Vikundi vitatu vya Ujasiriamali vya Kinamama, katika Ukumbi wa lango la Jiji, Magomeni Dar es Salaam, leo. Alikagua bidhaa hizo baada ya kuzungumza na Viongozi wa UWT Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Kuzaliwa kwa Jumuiya hiyo. (Picha na Bashir Nkoromo, CCM Blog) Picha zaidi Baada ya habari ifuatayo👇


Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, leo imeanza rasmi Maadhimisho ya kuzaliwa kwa jumuiya hiyo kwa kuongeza kasi ya kulivalia njuga suala la mikopo inayotolewa na serikali kupitia kila Halmashauri nchini.

Jumuiya hiyo imesema, imeamua kulivalia njuga suala hilo, kwa sababu ni jambo ambalo Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imelipa kipaumbele kwa lengo la kuwafanya wanawake nchini kujikomboa kiuchumi na hivyo kuweza kutoa mchango wao kwa jamii na familia zao badala ya kuwa tegemezi.

Akizungumza na vongozi wa UWT Wilaya ya Kinondoni, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga, amesema, UWT inao wajibu wa kusimamia suala hilo la mikopo kwa wananwake kwa sababu limo pia katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

"Wakati tunaadhimisha kuzaliwa kwa Jumuiya hii, kuna mambo ya kufanya, mojawapo ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020-2025, na katika ukaguzi huu, lengo letu kubwa ni kuangalia UWT katika mkoa wetu wa Dar es Salaam tupo kiwango gani katika mikopo hii ya asilimia 4 ya inayotolewa na Serikali inayoongozwa na jemedari, mwanamke mwenzetu Rais Samia Suluhu Hassam.

Kusimamia na kutekeleza Ilani hii kwetu sisi UWT ni jukumu la singi hasa katika kumuunga mkono mama yetu Rais Samia, kwa kuwa kufanikiwa kwa jambo hili la mikopo kwa kuwafikia wanawake wengi na kutoa tija, ndiyo manufaa yanayokusudiwa na Serikali ya CCM", amesema Masunga katika mkutano huo uliofanyika leo Ukumbi wa lango la Jiji, Magomeni, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Viongozi wa UWT mkoa wa Dar es Salaam katika Wilaya ya Kindondoni katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Jumuiya hiyo.

Masunga amewataka Wanawake wanapopata mikopo hiyo ambayo haina riba, kuitumia zivuri ili kukidhi lengo la Serikali, lakini pia amewahimiza kina mama wenye watoto wenye ulemavu kuwasaidia watoto hao ili nao wapate mikopo hiyo ya Halmashauri kwa kuwa nao wamo katika makundi yaliyopangiwa kuipata.

Amewataka pia kusadia vijana wanaostahili kupata mikopo hiyo, ili nao waipate, lakini akawataka kuwafundisha vijana hao ili wanapoipata mikopo waitumie kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali, na kuongeza kuwa miongoni mwa faida zitakazopatikana vijana hao wakipata mikopo na kuitumia vema itawafanya wajitegemee badala ya kuwa tegemezi kwa wazazi wao.

Akizungumzia maadhimisho hayo Masunga amesema, hayamaanishi UWT ni jumuiya changa bali ni ya miaka mingi tangu ilizaliwa mwaka 1964, wakati wa Katiba ya kwanza ya chama cha Tanganyika African National Union (TANU) chini ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere na kiongozi wa kwanza wa UWT akiwa Bibi Titi Mohammed.

Masunga amesema Maadhimisho yao yalianza rasmi jana, Oktoba Mosi na kwa mkoa wa Dar es Salaam, yataendelea hadi kesho kutwa Oktoba 4, 2021 huku akifafanua zaidi kwamba kitaifa yatafanyika Oktoba 23, 2021 katika Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga (Kulia) na Katibu wa Jumuiya hiyo mkoa wa Dar es Salaam Grace haule wakipokewa na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni Anna Hangaya, baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya CCM wilayani humo, kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuimarisha Jumuiya hiyo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya kuzaliwa Jumuiya hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya CCM wilayani humo, kuanza ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuimarisha Jumuiya hiyo, ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya kuzaliwa Jumuiya hiyo. Kulia ni Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga na Katibu wa UWT mkoa huyo Grace Haule (kulia) wakimsikiliza Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni Anna Hangaya kuhusu maendeleo ya Jumuiya hiyo Wilayani humo ikiwa ni pamoja na hali ya mikopo kwa Wanawake.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akizungumzia lengo la ziara yake katika Wilaya ya Kinondoni. Kulia ni Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga, na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule wakiwasili katika Ukumbi wa Lango la Jiji Magomeni kwa ajili ya kuzungumza na Viongozi wa UWT Wilaya ya Kinondoni na kukagua kazi za Wajasiriamali wanawake waliopata mikopo ya serikali kupitia Halmashauri.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni Anna Hangaya wakishangilia wakati wakilakiwa na  Wajumbe katika Ukumbi wa Lango la Jiji, Magomeni.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ukumbini. Kushoto ni Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akishauriana jambo na Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule (kushoto) baada ya kuwasili ukumbi wa Lango la Jiji, Magomeni kuzungumza na Viongozi wa UWT wilaya ya Kinondoni na kukagua vikundi vya Ujasiriamali vya Wanawake vilivyopata mikopo ya Serikali kupitia Halmashauri.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akisikilizwa na Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni Anna Hanagaya wakati akimwelekeza jambo wakati wa mkutano huo katika Ukumbi wa Lango la Jiji, Magomeni.
Viongozi mbalimbali wa UWT Wilaya ya Kinondoni wakiwa ukumbini wakati wa mkutano huo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga
Viongozi mbalimbali wa UWT Wilaya ya Kinondoni wakiwa ukumbini wakati wa mkutano huo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masung.
Viongozi mbalimbali wa UWT Wilaya ya Kinondoni wakiwa ukumbini wakati wa mkutano huo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masung.
Viongozi mbalimbali wa UWT Wilaya ya Kinondoni wakiwa ukumbini wakati wa mkutano huo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga.
Mmoja wa Viongozi wa UWT akifanya Utambulisho wa Viongozi mbalimbali wa UWT Wilaya ya Kinondoni
Viongozi mbalimbali wa UWT wakishangilia baada ya kutambulishwa
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule akizungumza kwenye kikao hicho katika Ukumbi wa Lango la Jiji Magomeni
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao hicho katika Ukumbi wa Lango la Jiji magomenii
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni Anna Hangaya akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam kuzungumza na viongozi katika kikao hicho
Kiongozi wa UWT alipokuwa akisoma risala kabla ya mgeni rasmi mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam kuzungumza
Mgeni rasmi akipokea risala
"UWT Hoyee, CCM Hoyee, Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia Suluhu Hassan Hoyeee.." Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akisalimia ukumbini kala ya kuanza kuzungumza na Viongozi wa UWT Wilaya ya Kinondoni katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akisisitiza jambo hasa kuhusu mikopo ya wanawake wakati akizungumza kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga akikagua bidhaa za vyungu wakati akifungua Vikundi vitatu vya Ujasiriamali vya Kinamama, katika Ukumbi wa lango la Jiji, Magomeni Dar es Salaam, leo. Alikagua bidhaa hizo baada ya kuzungumza na Viongozi wa UWT Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Kuzaliwa kwa Jumuiya hiyo.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kinondoni Anna Hangaya akimuungisha mjasiriamali kwa kununua bidhaa.
👆Mwenyekiti wa UWT mkoa wa dar es Salaam Florence Masunga na Katibu wa UWT mkoa huo Grace haule akikagua bidhaa mbalimbali za wajasiriamali hao👇



Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga akisaini kitabu cha wageni baada ya kufika kwenye maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali Tandale
👆Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga na katibu wa UWT mkoa huo Grace Haule wakifurahia bidhaa iliyonakishia bendera ya Taifa la Tanzania walipokuwa kwenye maonyesho ya wajasiriamali wanawake Tandale.👇

Mwenyekiti wa UWT  mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga akizungumza na Wanawake wajane ambao ni wajasiriamali waliopata mikopo ya Serikali kupitia Halmashauri ya Kinondoni, alipotembelea wajasiriamali hao Tandale👇

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga akiwa na Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kinondoni wakati wakitoka kukagua wajasiriamali wanawake, Tandale.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages