Katibu Mkuu, Prof. Msanjila akiaga baada ya kuzindua magari na mitambo hiyo.
Baadhi ya magari zaliyonunuliwa
Mitambo ya kisasa iliyonunuliwa
Baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa STAMICO wakiwa katika picha ya pamoja.
SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO), limenunua magari na mitambo ya uchimbaji na uchorongaji wa madini ili kuboresha na kuimarisha shughuli pamoja na kuanzisha migodi yake yenyewe.
Akizunguza wakati wa uzinduzi wa vitendea kazi hivyo,Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Prof. Simon Msanjila amesema kuwa magari na mitambo hiyo ya kisasa vimenunuliwa kutokana na vyanzo vya ndani vya shirika hilo.
Prof. Msanjila amesema vifaa vilivyozinduliwa vinaenda kuiwezesha STAMICO kuboresha utendaji kazi wake ambapo italiwezesha Shirika hilo kupata miradi mingine na kuitekeleza kwa ufanisi mkubwa.
“Ununuzi wa Mitambo hii utaiwesha STAMICO kutelekeza miradi na kandarasi mbalimbali iliyonayo pamoja na miradi mingine itakayo pata ambapo itasaidia kuzalisha kwa faida na kutoa gawio kwa Serikali”, amesema Prof. Msanjila.
Awali, Prof Msanjila alilifunga Baraza la 8 la wafanyakazi wa STAMICO na kuwataka wafanyakazi wote wa Shirika hilo kuendelea kushirikiana ili kufanikisha Malengo ya Shirika hilo.
Katika Baraza hilo, Prof. Msanjila amesema kuwa, makubaliano ya kikao hicho ni kufuatilia utekelezaji wa malengo yaliyojadiliwa katika kikao kazi hicho na kusisitiza ufuatiliaji wa yote yaliyozungumzwa.
Aidha, Prof. Msanjila amewataka watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la Sensa linalotarajia kufanyika Oktoba 2022 huku akiwahimiza watanzania wote kujitokeza kupata chanjo ya Uviko-19 kwani ugonjwa huu upo.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse ameeleza utekelezaji wa bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/2021 huku akizungumzia malengo ya kukusanya mapato kwa Mwaka wa Fedha 2021 kuwa, Shirika lilipangiwa kukusanya shilingi billion 19 .4 ambapo walivuka lengo kwa kukusanya bilioni 19.6 sawa na asilimia 101.
Dkt. Mwasse amesema, Shirika limeweza kununua magari na mitambo ya kisasa kwa ajili ya kuboresha shughuli za uchimbaji na uchorongaji wa madini ambapo kiasi cha shilingi bilioni 1.7b kilitumika.
Dkt. Mwasse ameongeza kuwa Shirika lina lengo la kujiimarisha zaidi katika kuendesha miradi yake na kutafuta zaidi kandarasi ili kijiongezea mapato na kulipa baadhi ya madeni ambayo Shirika ilikuwa inadaiwa.
Dkt. Mwasse amesema, Shirika limeonesha viashiria vya kujiendesha kwa kujitegemea ambapo Shirika limepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 76.2 kutoka vyanzo vyake vya ndani ambapo ndani ya miaka mitatu iliyopita Shirika lilikuwa linakusanya kiasi cha shilingi bilioni 1.3, katika miaka mitatu iliyopita Shirika lilikuwa linaitegemea Serikali kwa asilimia 87 Mwaka wa Fedha 2021/2022 Shirika linaitegemea Serikali kwa asilimia 13.
“Shirika limepanga kununua mitambo 5 ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo ili tuweze kuwasaidia wachimbaji wadogo ambao sisi kama Shirika ndiyo walezi wao, na tuna mpango wa kuanzisha Vituo vingine viwili vipya vya Mfano ili kuiendeleza Sekta yetu ya Madini,” amesema Dkt. Mwasse.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇