LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 24, 2021

RAIS SAMIA AMUAGA RAIS WA BURUNDI

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakizungumza katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 wakati wa Mhe. Ndayishimiye alipokua akiondoka kurejea Nchini Burundi baada ya kukamilisha ziara yake hapa Nchini.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakiangalia vikundi mbalimbali vya ngoma za asili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 mara baada ya Rais huyo wa Burundi Mhe. Ndayishimiye kuhitimisha zira yake nchini na kurejea Burundi. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Mke wa Rais Evareste Ndayishimiye wa Burundi kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 wakati Mhe. Ndayishimiye alipokua akiondoka kurejea Nchini Burundi baada ya kukamilisha ziara yake leo tarehe 24 Oktoba, 2021. kulia ni Rais wa Ndayishimiye wa Burundi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 wakati Mhe. Ndayishimiye alipokua akiondoka kurejea Nchini Burundi baada ya kukamilisha ziara yake leo tarehe 24 Oktoba, 2021. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages