LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 13, 2021

NMB YATANGAZA WASHINDI BONGE LA MPANGO AWAMU YA PILI

 ADVERTISEMENT

Benki ya NMB imetangaza washindi katika droo ya kwanza ya kampeni ya Bonge la Mpango awamu ya pili.Washindi hao wametokana na kuwekeza kiasi cha kuanzia Tsh.100,000 na kuendelea.

Akitangaza  washindi hao mbele ya waandishi wa habari leo Oktoba 13,2021, Meneja Mwandamizi wa Wateja Binafsi, Ally Ngingite amesema benki ya NMB imezingatia vigezo vyote vilivyowekwa kisheria katika kuwapata washindi katika droo hiyo.

Ngingite ameongeza kuwa lengo la kampeni ya Bonge la Mpango awamu ya pili ni kuwahamasisha wateja wa NMB na watanzania kwa ujumla kujua faida za kibenki.

” Leo tunatangaza washindi 12 wa droo ya kwanza ya kampeni ya Bonge la Mpango awamu ya pili, lengo la NMB benki ni kuhamasisha wateja kujua huduma za kibenki” Amesema Ngingite.

Kwa upande wake mkaguzi wa michezo ya kubashiri kutoka Bodi ya Michezo ya Kubashiri Tanzania, Joram Mtafya, ambaye amesimamia droo hiyo pamoja na kutangazwa kwa washindi amesema bodi ya kubashiri itaendelea kuzingatia vigezo muhimu ikiwa ni pamoja na mshiriki kupigiwa simu mara tatu.

Miongoni mwa washindi waliotangazwa katika droo hiyo ni pamoja na Kuluthum Sadiki Chande kutoka Ifakara mkoani Morogoro, Justine James Yona na George Sabiano Obila kutokea Rorya mkoani Mara.

Kampeni ya Bonge la Mpango itakuwa ikifanyika kila mwezi ambapo wateja wa benki ya NMB watakaowekeza kiasi cha kuanzia Tsh.100,000 watakuwa washiriki wa droo husika na miongoni mwao kuibuka washindi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages