LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 20, 2021

MALAGISHIMBA ATEULIWA KUWA MJUMBE WA KAMATI YA UCHUMI NA FEDHA JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA ILALA

Na Heri Shabani, CCM Ilala
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni katika Jimbo la Ukonga Daiel Malagashimba ameteuliwa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala kuwa Mjumbe wa Kamati ya Uchumi na Fedha katika Jumuiya hiyo.

Akitoa Shukurani kufuatia uteuzi huo ulioanza tangu Septemba 29, 2021, leo Malagashimba amesema anakishukuru Chama cha Mapinduzi (CCM) na Jumuiya ya Wazazi wilaya llala kwa kumwamini na kumpa nafasi hiyo.

Malagashimba amesema atafanyakazi kwa juhudi, maarifa na kwa weledi katika kujenga Chama na Jumuiya zake kupitia nafasi hiyo aliyoteuliwa.

"Nawashukuru viongozi wangu wa Jumuiya ya Wazazi kunipa cheo hiki kizito, nitashirikiana nanyi katika kazi za Jumuiya yetu na kuhakikisha Jumuiya inafikia malengo yake "alisema Malagashimba.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni katika Jimbo la Ukonga Daiel Malagashimba

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages