LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 26, 2021

MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO KUWAONGOZA WANARIADHA ZAIDI YA 2000 KWENYE MBIO YA MAZINGIRA MARADHONI NOVEMBA 14

 
    Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango anatarajia kuwaongoza wanariadha zaidi ya 2000 kwenye mbio ya Mazingira marathoni itakayofanyika Novemba 14 kwa mara ya kwanza nchini.

Wanariadha wa ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kukimbia kwenye mbio hiyo itakayoanzia na kumalizikia kwenye viwanja vya green ground maarafu kama uwanja wa farasi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa mbio hiyo, Dr. Amon Mkoga amesema kuwa mbio hiyo inalenga kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuhifadhi mazingira nchini.

Amesema wanariadha watachuana katika mbio za nusu marathoni (kilomita 21), kilomita 10 na kilomita tano ambayo makamu wa rais pia atakimbia mbio hiyo.

"Maandalizi yameanza kwa wakimbiaji kujiandikisha kwa njia ya mtandao, mbio hii mbali na kuhamasisha utunzaji wa mazingira ambao utakwenda sanjari na upandaji miti, pia utasaidia vifaa vya uzazi kwa wa kina mama.

"Katika utoaji vifaa, tunashirikiana na Tasaf na vifaa hivi vitatolewa kwa kaya masikini kwenye maeneo mbalimbali nchini," amesema.

Mmoja wa wasanii kwenye mbio hiyo, Haruna Kahena 'Inspector Haroun' ambaye ni miongoni mwa watakaokimbia mbio za kilomita 5 alisema anatamani mabingwa wote watoke nchini.

Amesema mbali na mbio hiyo kuwashindanisha wakimbiaji nyota nchini, lakini pia ni sehemu ya mazoezi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages