LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 17, 2021

KATIBU MKUU WA CCM DANIEL CHONGOLO AELEKEZA KAMATI ZA SIASA ZA WILAYA NA MIKOA, NA WIZARA ZOTE USIMAMIZI NA MGAWANYO WA FEDHA ZA UVIKO 19

 


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo  ametoa maelekezo kwa Kamati za Siasa za Mikoa na Wilaya nchi nzima kuhakikisha zinasimamia fedha za UVIKO 19 shilingi Trilioni 1.3 zinazopelekwa katika maeneo yao, sambamba na wizara zote kuweka mgawanyo wa wazi wa fedha hizo kama ilivyofanyika Katika wizara ya TAMISEMI.

Katibu Mkuu ametoa maelekezo hayo leo tarehe 17 Oktoba, 2021 katika ziara ya kikazi ya Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Mhe. Samia Suhulu Hassan Mkoani Arusha.

"Kamati zote za siasa ngazi za Mikoa na Wilaya nchi nzima, popote pale fedha zitakapothibitika zimepotea na ninyi mtawajibika kwa kutosimamia fedha hizo kwenye maeneo yenu, kwa sababu, kwa kutofanya hivyo tutakuwa tunaikwamisha Ilani yetu wenyewe kutekelezwa katika kiwango chenye tija." Katibu Mkuu CCM Ndg. Chongolo

Wakati huo huo, Katibu Mkuu ameipongeza Wizara ya TAMISEMI kwa kutoa mchanganuo wa fedha za UVIKO 19, ilizopokea katika mgao wa kila wizara  ambapo amezitaka wizara zote kutoa mchanganuo wa matumizi ya fedha hizo kwa kufuata mfano ilivyofanyika kwa wizara ya TAMISEMI inayoongozwa na Mhe. Ummy Mwalimu. 

Aidha, Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Rais Samia kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya na kuwaomba wanaArusha na watazania wote kuendelea kumuunga mkono Mhe. Rais Samia pamoja na Serikali anayoiongoza kwani imedhamiria kufanya mambo makubwa na yenye tija kwa wananchi wote.

Imetolewa na;

Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages