Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Dkt Fatma Mganga akizungumza kwa kutoa neno la utangulizi kwa kutoa salamu za ukaribisho na lengo la Mkutano wa Kamati ya Afya ya Msingi kuhusu Kinga na Chanjo dhidi ya UVIKO-19 kwa mkoa huo, lakini pia kuelezea Mpango jamii shirikishi na harakishi wa chanjo hiyo. Mkutano huo umefanyika leo Oktoba 18 2021, Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa huo.
Mkoa wa Dodoma ambao umekuwa wa tatu nchini kumaliza haraka dozi za awamu ya kwanza za JJ kutoka Marekani, Tayari umepokea tena zaidi ya dozi 50,000 aina ya Sinopharm kutoka China. Mikoa iliyoongoza ni Dar es Salaam na Kilimanjaro.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir Shekimweri akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Best Magoma akielezea ufanisi wa chanjo ya awamu ya pili ya Sinopharm kutoka China kwamba imefanyiwa utafiti wa kutosha na wataalamu wa kitanzania hivzo wananchi wajitokeze kwa wingi kuchanjwa.
Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Dodoma,Francis Bujiku akielezea mpango mkakati wa kuongeza kasi ya uchanjaji wa chanjo ya UVIKO -19.
Afisa Afya Mkoa wa Dodoma, Nelson Rumbeli akifafanunua jambo wakati wa mkutano huo.
Sheikh wa Mkoa wa Dodoma akitoa ushauri kwa uongozi wa Dodoma kuwashirikisha wataalamu wa afya kutoa elimu kuhusu Chanjo ya UVIKO 19 misikitini na makanisani pamoja na kuweka vibanda vya kufanyia chanjo.
Sehemu ya washiriki wakiwa katika mkutano huo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video hapa chini, Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Dodoma, Francis Bujiku na Katibu Tawala wa mkoa huo, Dkt Fatma Mganga wakielezea kuhusu mpango mkakati huo.....
Imeandaliwa na Richard MwaikendaMhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇