LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 5, 2021

DK. MPANGO ANOGESHA SHEREHE ZA KILELE CHA MAADHIMISHO YA WIKI YA UWT KWA MKOA WA DAR ES SALAAM, AWAFUNDA MAZITO UWT

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam,  Florence Masunga akimpatia zawadi ya chungu cha kisasa Mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango wakati wa Sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya UWT kwa mkoa huo,zilizofanyika leo katika Ukumbi wa PTA, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Vyungu hivyo vimetengenezwa na Wajasiriamali Wanawake ambao wamepata mikopo ambayo hutolewa na Serikali bila riba kupitia Halmashauri zote nchini.

 

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, PTA

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amenogesha kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam, baada ya kuhudhia akiwa mgeni rasmi na kuwafunda kwa maneno mazito wanachama wa Jumuiya hiyo.

Dk. Mpango ambaye ndiye Mlezi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, kihutubia katika Sherehe za Kilele hicho zilizofanyika katika Ukumbi wa PTA kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Kimataifa ya Baashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), kwanza  amewashuru nawake woten chini kupitia Jumuiya hiyo ya UWT kwa kuwa mstari wa mbele katika kukiimarisha CCM kwa uaminifu mubwa.

Amesema  pia anawashukuru kwa kuwa wameedelea kuliombea aifa amani na mshikamano pamoja na kuiombea Serikali na viongozi wake na kuisifu  UWT kuwa ndiyo Jumuiya kubwa ndani ya CCM kwa kuwa ndiyo yenye wanachama wengi hivyo CCM inatambua mchango huo katika ushindi wa chaguzi zake zote.

Makamu wa Rais amesema kutokana na wingi wao na ukubwa kuliko Jumiya nyingine za CCM UWT wanastahili na wanapaswa kuwa sauti ya Wanawake katika uwezeshaji wa wanawake kiuchumi na kupiga vita ukatili na unyanyasaji wa wanawake katika jamii.

Amebainisha kuwa mchango unaotolewa na wanawake katika malezi, lishe bora, kulinda maadili katika jamii pamoja na ujenzi wa uchumi ni mkubwa na hivyo kuwataka kuendelea kuwa kichocheo cha kuijenga Tanzania imara katika nyanja hizo hasa za kijamii na kiuchumi.

Aidha amewaasa UWT kufanya juhudi za kuongeza wanachama, kuhimiza uhai wa wanachama, kufanya vikao vya Jumuiya hiyo, kuwa mstari wa mbele katika ziara za ukaguzi wa uhai wa Chama, kulinda amani ya nchi pamoja na kuepuka migogoro ndani ya Jumuiya hiyo.

Akizungumzia kuhusu Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Oktoba mwakani na kuhusu mapambano dhidi ya Maradhi ya Uviko 19, Dk. Mpangoa amewasihi UWT  kujitokeza pamoja na kuelimisha wananchi kushiriki kati kasensa hiyo na pia kuhimiza wananchi katika kujinga na Uviko 19, hasa kwa kuhimiza watu kupata chanjo.

Awali akisoma risala kwa niaba ya wanawake wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Katibu wa UWT wa mkoa huo Grace Haule, amesema hadi UWT inatimiza miaka 44 tangu kuanzishwa kwake imeshiriki kikamilifu kutoa mchango wake katika ujenzi wa taifa katika sekta mbalimbali zikiwemo za Afya, Elimu, Miundombinu, Nishati na Miundombinu ya Maji na kuipongeza erikai kwa kuboresha sekta hizo kwani zimekuwa na msaada mkubwa kwa wanawake hapa nchini.

Grace amesema wanawake mkoa wa Dar es salaam anatambua juhudi kubwa zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea wananch imaendeleo,hivyo wanaunga mkono juhudi hizo.

Katika Mkutano huo UWT mkoa wa Dar es salaam wamewasilisha pia ombi kwa mke wa Makamu wa Rais Mama Mbonimpaye Mpango kuwa mlezi wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Dar es Salaam ambapo mkewa Makamuwa Rais ameridhia ombi hilo. 

Matukio katika Picha👇

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, akisalimiana na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, Florence Masunga, alipolakiwa na Viongozi mbalimbali baada ya kuwasili kwenye Sherehe za Maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya UWT kwa mkoa wa Dar es Salaam, zilizofanyika katika ukumbi wa PTA, Barabara ya Kilwa dar es Salaam. Kushoto ni Mama Mbonimpaye Mpango, na Watatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Kate Kamba na kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam Shaibu Akwilobe.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akiwa amesimama na viongozi meza kuu baada ya kuwasili. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akiwa ameketi baada ya kuwasili ukumbini. Kushoto ni Mama Mbonimpaye Mpango na katikati ni Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga.
Katibu wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Grace Haule akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akiwa amesimama tayari kuhutibia, lakini akamwalika kwanza mkewe Mama Mbonimpaye Mpango
Mama Mbonimpaye Mpango akizungumza.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam akimpongeza Mama Mbonimpaye aliporejea mezani baada ya kuzungumza
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akiendelea kuzungumza baada ya kumtambulisha Mama Mbonimpaye Mpango.
Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Dar es Salaam ambao ni Makamisaa wa CCM wakiwa kwenye hafla hiyo
Wakuu wa Wilaya za mkoa wa Dar es Salaam ambao ni Makamisaa wa CCM wakiwa kwenye hafla hiyo
Baadhi ya wabunge wanawake kutoka mkoa wa Dar es Salaam (Viti vya Mbele) wakiwa kwenye hafla hiyo
Waalikwa wakiwemo viongozi wa UWT na CCM wakiwa kwenye hafla hiyo
Waalikwa wakiwemo viongozi wa CCM na Wabunge wakiwa kwenye hafla hiyo
Waalikwa wakiwemo viongozi wa UWT na CCM wakiwa kwenye hafla hiyo.
Waalikwa wakiwemo viongozi wa UWT na CCM wakiwa kwenye hafla hiyo.
Waalikwa wakiwemo viongozi wa UWT na CCM wakiwa kwenye hafla hiyo.
Dk. Mpango akirejea meza kuu baada ya kuhutibia kwenye hafla hiyo.
Dk. Mpango akipongezwa na Mwenyekiti wa UWT Dar es Salaa Florence Masunga
Dk. Mpango akiwa bado amesimama meza kuu wakati akishangiliwa baada ya hotuba yake
Dk, Mpango akiwa ameketi na Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam, wakati burudani ya ngoma ikianza
Dk. Mpango (kulia) akienda kutuza, baada ya kufurahishwa na Burudani ya ngoma hiyo
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akicheza kidogo ngoma ngoma na wasanii baada ya kuvutiwa
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam Florence Masunga na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla wakienda kuwatuza wasanii kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Dar es Salaam akiwatuza wasanii wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya Viongozi wa UWT wakiwatuza wasanii
Baadhi ya viongozi wa UWT wakiwatuza wasanii. Anayerusha pesa ni Mjumbe wa NEC Angel Akilimai.
Wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam Janeth Mahawanga na Janeth Masaburi wakitoka kutuza wasanii wakati wa hafla hiyo.
Kijana wa Ngoma za asili akionyesha uhodari wake wa kuchezea nyoka wakati wa hafla hyo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akiendelea kupewa urudani ya ngoma za asili ukumbini.
Katibu wa UWT wa mkoa wa Dare Salaam akimwalika jukwaani kuzungumza Mjumbe wa NEC, Angel Akilimali.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Angel Akilimali akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waUWT na CCM mwishoni mwa hafla hiyo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango na Mama Mbonimpaye Mpango wakiaga wakati wakiondoka ukumbini mwishoni mwa hafla hiyo.

©2021 CCM Blog/Bashir Nkoromo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages