CCM Blog, Tegeta
Katika jitihada zake za kuiinua Jamii ili watu waweze kuishi maisha yamayostahili, Kanisa la Mungu Baba limeandaa Ibada ya 'kufuta ajali' za Bodaboda ambazo jamii imekuwa ikizishuhudia kwa miaka kadhaa sasa tangu Serikali iliporuhusu vyombo ya Pikipiki kutumika kusafirisha abiria Nchini.
Baba Halisi wa Uzao ambaye ndiye Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo lenye Makao yake Tegeta jijini Dar es Salaam, amesema katika taarifa yake kuwa, Ibada hiyo ya aina yake, itafanyika keshokutwa Jumapili, Oktoba 24, 2021 katika Makao Makuu ya Kanisa hilo.
Baba Halisi amesema, ameshawapa mwaliko waedesha Bodaboda bila kubagua maeneo waliko, kuhudhuria Ibada hiyo muhimu.
Ibada hiyo ni mwendelezo wa Ibada ambazo zimekuwa zikifanywa na Kanisa hilo zikiwa zinaielenga jamii moja kwa moja katika kuwavusha watu wa aina mbalimbali kutoka katika majanga na kuingia katika mwenendo uliobarikiwa na Mungu Baba katika shughuli zao za Uzalishaji.
Moja ya Ibada inayilingana na hiyo ya Ijumapili ya keshokuwa ni ile iliyofanyika Jumapili iliyopita (Oktoba 17, 2021) katika Kanisa hilo iliyokuwa Ibada Maalum ya Kuwabariki Waandishi wa Habari, ambayo iliweza kuhudhuriwa na Waandishi na watangazaji zaidi ya 50 wa Vyombo mbalimbali vya Habari nchini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇