LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 26, 2021

TAMASHA LA MICHEZO LA NHIF LAFANA DODOMA+video

Wachezaji wa timu ya Netiboli ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) waliovaa nyekundu wakichuana na timu ya Chuo cha Mipango wakati wa Tamasha la Michezo  la NHIF na  Wanahabari lililofanyika Septemba 25, 2021 kwenye viwanja vya Kilimanj jijini Dodoma.

Waandishi wa Habari kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani walishiriki Tamasha hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabir  Shekimweri akihutubia wakati wa ufunguzi wa Tamasha hilo ambapo alihimiza watu kujenga tabia ya kufanya maoezi kupitia michezo. Shekimweri alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Amthony Mtaka.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Shekimweri akipiga mpira ikiwa ni ishara ya kufungua tamasha hilo upande wa soka.
Rais wa Klabu za Habari za Mikoa Tanzania, Deo Nsokolo (kulia) akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Shekimweri (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga. 
Shekimweri akikagua timu ya mpira wa miguu
Shekimweri akitoa neno kwa wachezaji wa timu ya Netiboli ya NHIF.
Shekimweri akitoa neno kwa wachezaji wa timu ya Netiboli ya Chuo cha Mipango.
Shekimweri akifungua  mchezo wa  Netiboli.
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa NHIF, Anjela Mziray (kushoto) akiwa miongoni mwa washabiki wakishuhudia mchezo wa netiboli.
Shekimweri akikagua timu za mpira wa wavu


 Patashika ya mchezo wa Netiboli kati NHIF na Mipango.

PICHA YOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau nakuomba uendelee kuona yaliyojiri  katika Tamasha hilo ambapo pia utamsikia Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Jabiri Shekimweri akihutubia wakati wa ufunguzi wa Tamasha ...

Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM 
0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages