LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 20, 2021

SKAUTI WA KIKE TGGA WAFURAHIA KUVINJARI HIFADHI YA TARANGIRE+video

Askari Uhifadhi Daraja la Kwanza ,Ally Omary  wa Hifadhi ya Taifa  Tarangire  akielezea kuhusu utaratibu wa malipo na maelekezo muhimu wakati wa kutembelea Hifadhi hiyo wakati wa ziara ya viongozi wa Skauti wa Kike wa Chama cha Tanzania Girl Guides (TGGA), mwishoni mwa wiki.

 Mwenyekiti wa TGGA, Prof. Martha Qorro akielezea lengo la ziara hiyo iliyofanyika baada ya kuhudhuria Kambi ya mafunzo elekezi kwa viongozi wapya wa chama hicho, Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Wakiwa ndani ya gari kuelekea mbugani



Tembo akiwa na mtoto


                                       Digidigi
                                Nyumbu

Watalii wa ndani yaani wazawa wakiangalia wanyama wakiwa ndani ya gari

                                  Pundamilia
                                          Twiga
Watalii wa ndani kutoka TGGA wakipiga picha wanyama waliowaona
                                             Tembo
Mabango yenye maumbile ya wanyama  yakiwa yameandikwa kuelekeza maeneo karibu na mapokezi ya Hifadhi ya Tarangire.  


Baadhi ya watalii wa ndani wa TGGA kutoka Zanzibar.
                                 Ofisi za Tarangire

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Na Richard Mwaikenda VIONGOZI wapya wa Chama Cha Skauti wa Kike cha Tanzania Girl Guides (TGGA), wamefurahia kutembelea Hifadhi yaTaifa ya TARANGIRE ambapo walijionea ndege na wanyama wa aina mbalimbali. Ziara hiyo ya kutembelea Tarangire iliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa TGGA, Profesa Martha Qorro ambapo zaidi ya viongozi wapya 150 na sekretarieti walipata guess hiyo. Viongozi hao walipata wasaa huo wa kuvinjari katika hifadhi hiyo mwishoni mwa wiki wakitokea Kambi ya Mafunzo elekezi ya siku 6 katika Shule ya Sekondari ya Fundi Moshi, Mkoani Kilimanjaro. Walipofika walilakiwa kwa bashasha na watumishi wa Tarangire wakiongozwa na Askari Uhifadhi Daraja la Kwanza ,Ally Omary  ambao walielezwa taratibu zote za malipo na masharti yanayopaswa kufuatwa wakati wa kutembelea Hifadhi hiyo. Baada ya hapo waliruhusiwa kupanda kwenye magari kwenda kutembelea Hifadhi huku kila gari likiwa na muongoza watalii mahsusi kutoa maelezo na maelezo kuhusu tabia za wanyama na ndege waliobahatika kuwaona. Wengi wa viongozi hao kutoka mikoa 20 ya Tanzania Bara na Visiwani walifurahishwa sana na ziara hiyo kwani baadhi yao ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kutembelea mbuga na kuwaona live ndege na wanyama. Walibahatika kuwaona Swala, Tembo, Twiga, Pundamilia, Nyumbu, Digidigi, Mbuni, Karani ndege, Hondohondo na wengineo. Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video Askari Uhifadhi Daraja la Kwanza ,Ally Omary Tarangire akielezea umuhimu wa wazawa Kujenga tabia kutembelea Hifadhi kwa gharama nafuu, lakini pia Profesa Martha Qorro wa TGGA akielezea lengo la ziara hiyo pamoja baadhi ya viongozi wakielezea jinsi ziara hiyo ilivyowafurahisha....


Imeandaliwa na Richard Mwaikenda 
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages