LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 7, 2021

PSSSF YATAJWA KUWA MIONGONI MWA TAASISI ZA MWANZO KUTUMIA MFUMO WA PAMOJA WA UTOAJI HUDUMA NCHINI

Na Mwandishi Maalum, Dar es Salaam
MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ni miongoni mwa Taasisi za mwanzo kujiunga na Mfumo wa Utoaji Huduma wa Pamoja wa Serikali (One Stop Service Centre) ambao Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameuzindua leo Septemba 6, 2021 jijini Dar es Salaam.

WAZIRI Mkuu amezitaka Taasisi nyingine za Serikali ambazo bado hazijajiunga na Mfumo huo unaoratibiwa na Shirika la Posta Nchini, kuhakikisha zinajiunga ndani ya mwaka huu wa fedha wa 2021/2022.

“Mradi huu unaenda kubadilisha namna ya utoaji huduma bora, ni muhimu kuharakisha na kuhakikisha kwamba unafanikiwa, hivyo basi nazielekeza taasisi zote zinazotoa huduma kuongeza kasi ya kujiunga na Utaratibu wa Utoaji Huduma wa Pamoja.” Alisisitiza.

Mapema, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndungulile alizitaja Taasisi ambazo tayari zimeshaanza kutoa huduma kupitia mfumo huo kuwa pamoja na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Vizazi na Vifo (RITA), Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA),  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Idara ya Uhamiaji, BRELA, Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NHIF) na Benki ya CRDB.

Dk. Ndungulile alisema, kwa kuanzia Mfumo huo tayari umezinduliwa kwenye mikoa ya Dodoma na Dar es Salaam na kwamba lengo ni kufikia mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Akizungumza baadaye na mwandishi wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSSSF C.P.A Hosea Kashimba alisema, Taasisi yake iliamua kujiunga mara moja na Mfumo huo kwa sababu Mfuko unawajali Wanachama na Wateja wake.

“Tuliona utaratibu huu ni mzuri, utapelekea kumuhudumia mwanachama kwa haraka lakini pia kuondoa usumbufu ambao pengine mwanachama anaweza kukutana nao hivyo anaweza akafika hapa na kuhudumiwa na kama kuna taarifa zinahitajika kutoka Taasisi nyingine Taasisi hizo nyingine ziko hapa ikiwemo NIDA, RITA na Taasisi ambazo tunashirikiana katika kutoa huduma.” Alisema C.P.A Kashimba.

Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, C. P. A Hosea Kashimba (mbele) akiwa amesimama pamoja na wakuu wengine wa Taasisi za Umma ambazo tayari zimeanza kutoa huduma kwenye kituo hicho kilichoko Posta Mpya jijini Dar es Salaam.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) C.P.A Hosea Kashimba (Kushoto). wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Pamoja wa Utoaji Huduma Taasisi za Umma unaoratibia na Shirika la Posta nchini. Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mkuu Septemba 6, 2021 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndungulile (wapili kushoto) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso muda mfupi kabla ya uzinduzi huo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainabu Chaula (kushoto) na Naibu Katibu Mkuu wake, Dkt. Jimmy Yonazi (katikati) wakimsikiliza Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Bw. Macrice Daniel Mbodo
C.P.A Kashimba (kulia) akizungumza na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Dkt. Dkt. Francis Michael (katikati) na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Dotto James.
C.P.A Kashimba akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (kulia) akimsikilzia Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mashomba kuhusu namna Mfuko huo unavyohudumia wanachama wake kwenye kituo hicho cha huduma ya pamoja
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, C.P.A Hosea Kashimba (kushoto) akimsikiliza Meneja wa PSSSF, Bw. Rajabu Kinande

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages