LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 3, 2021

MAANDALIZI YA MKESHA MKUBWA WA KULIOMBEA TAIFA YAPAMBA MOTO

Wajumbe wa Kamati za Kitaifa za Mkesha Mkubwa wa Kitaifa wakiomba wakati wa kikao cha maandaliyi  jzya mkesha huo utakaofanyika Dodoma Desmba 31 2021. Kushoto ni Mwenzekiti wa  Askofu Godfery Malassy.
Mwenzekiti wa Taifa wa mkesha huo, Askofu Malassy akizungumza wakati wa kikao hicho na kuitaja Tanzania kuwa ni nchi ya kipekee ulimwenguni na kwamba imechorwa kwenze kiganja cha Mungu ndiyo maana imekuwa nchi ya Amani na Utulivu.



Mratibu wa Tamasha hilo, Debora Malassy akiomba wakati wa kikao hicho kilichofanyika Chuo cha Ufundi VETA Dodoma
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi ya mkesha huo.

Ilikuwa ni kuimba na kumuabudu Mungu wakati wa kikao hicho cha maandalizi.




PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Na Richard Mwaikenda, Dodoma

MAANDALIZI ya Mkesha mkubwa wa Kitaifa wa kuliombea Taifa na viongozi  ili Tanzania iwe ya amani na utulivu litakalofanyika Desemba 31 yameanza.

 

Maandalizi hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa Taifa wa Tamasha  hilo la Dua Maalumu kwa Taifa, Askofu Godfrey Malassy amesema katika kikao cha maandalizi , kuwa mkesha huo utafanyika tarehe hiyo kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma. Tamasha hilo lililoanyishwa 2009 Kwa Dodoma litakuwa la 8.


Ametoa rai kwa wananchi bila kujali itikadi ya dini wala vyama  kujitokeza kwa wingi siku hiyo kwa kushiriki kuomba na kuwa shahidi wa matendo makuu, juu ya Taifa la Tanzania kuwa la amani na utulivu.


Sote tunafahamu Taifa letu limekuwepo miaka yote na limekuwepo na amani ya kudumu lakini watu wengi hawajui siri yake ni nini? Nchi nyingi duniani leo wanauliza Tanzania kuna nini inakuwaje inakuwa na amani ya kudumu? wakati majirani zetu  hakuishi kukucha ni vita?


Si kwamba Tanzania na majeshi imara, wananchi, lakini hiyo si sababu, nchi nyingine pia zina majeshi lakini ni vita asubuhi na jioni. Nitawambia  siri hiyo, ni kwamba Tanzania imechorwa kwenye kiganja cha Mungu, Tanzania imewekwa katika moja ya majukumu ya siku ya mwisho.


Ili kuthibitisha maneno hayo , Askofu Malassy amewaomba watanzania kusoma neno la Mungu kwenye Biblia kwa kufunua Sura  18 mstari wa 1-7  ambayo inaeleza nchi ambayo ilipandisha bendera mlimani na kwamba utabiri huu ulitokea miaka 600 kabla ya kuzaliwa Kristo. Wakati wa Uhuru 1961 Tanzania ilipandisha Bendera ya Taifa katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro.



Amesema kwa uthibitisho huo Tanzania ni nchi ya kipekee ulimwenguni hivyo kila mmoja ana wajibu wa kuliombea taifa , Rais na Serikali ili wanapokuwa wanatawala watawale kwa kichwa cha Mungu ili amani na utulivu uendelee


Askofu Malassy amesema pia kuwa madhumuni  mengine ya mkesha huo ni kuomba kuhakikisha Mungu anaiponya Tanzania na ugonjwa wa Corona, kama alivyoliponya huko nyuma ambapo pia aliwataka watanzania kuchukua tahadhari nyingine zaidi.


Kikao hicho cha maandalizi kilihudhuriwa pia na viongozi wengine wa kamati ya maandalizi ambao ni, Juliana Manyerere, Mchungaji Rose Amani, Rose Massawe na Debora Malassy na wengineo.


 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages