Kamonga akiangalia makaa ya mawe ambayo tayari yameshachimbwa katika mgodi huo.
Kamonga akionesha moja ya vipande vya mkaa huo.
Akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa mgodi huo.
Eneo la Mgodi huo wa makaa ya mawe.
Na Richard Mwaikenda, Ludewa
MBUNGE wa Ludewa ametembelea usiku Mgodi mpya mkubwa wa makaa ya mawe uliogunduliwa katika eneo la Kitongoji cha Ndambasi, Kijiji cha Masimavalafu, Kata ya Ibumi, wilayani Ludewa, Njombe kujionea jinsi unavyofanya kazi.
Kilomita moja kabla ya kuingia eneo la mgodi, karibu na Mto Liugai, Kamonga alikuta lundo la makaa ya mawe zaidi ya tani 700 hali ambayo ilimpa matumaini kuwa kweli kuna uchimbaji wa madini hayo.
Alipofika eneo la mradi huo alikaribishwa na Meneja Mwendeshaji wa mgodi huo, Vincent Malima na hatimaye kutambulishwa kwa wafanyakazi takribani 20 ambao aliambiwa asilimia kubwa wameajiriwa kutoka vijiji jirani na mgodi huo.
Malima alieleza kuwa kampuni tayari imeshapata kibali cha kuendesha mradi huo na kwamba wakishaingiza mitambo ya kisasa watakuwa wanachimba takribani tani 100,000 kwa mwezi ambazo tayari zimepata wateja.
"Tupo tayari kulipa kodi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na Serikali Kuu,"amesema Malima.
Ili kurahisisha uendeshaji wa mradi huo mkubwa, Malima ameiomba Serikali kujenga miundombinu ya barabara na umeme kwenda kwenye mgodi.
Mdau, ili nisikuondolee uhondo nakuomba uendelee kusikiliza/ kuona kupitia clip hii ya video, Mbunge Kamonga akitembelea mgodi huo, Meneja Malima akielezea kuhusu mradi huo na baadhi ya wafanzakazi wakielezea furaha ya uwepo wa mradi huo na faida watakazopata......
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇