LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 22, 2021

DKT MABULA AAGIZA KUMALIZWA MGOGORO WA ARDHI WANANCHI NA MAGEREZA KONDOA

 

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza katika kikao na viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo tarehe 21 Sept 2021 akiwa katika ziara ya siku tano mkoani Dodoma.

Mkuu wa wilaya ya Kondoa Dkt Khamis Mkanachi akizungumza katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo tarehe 21 Sept 2021 akiwa katika ziara ya siku tano mkoani Dodoma.

Kamishna wa Ardhi Msaidizi Thadei Kabonge akizungumza katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo tarehe 21 Sept 2021 akiwa katika ziara ya siku tano mkoani Dodoma.

 Mbunge wa jimbo la Kondoa Mjini Ally Makoa akizungumza katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo tarehe 21 Sept 2021 akiwa katika ziara ya siku tano mkoani Dodoma.

 Mbunge wa jimbo la Kondoa Mjini Ally Makoa akizungumza katika kikao kati ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma leo tarehe 21 Sept 2021 akiwa katika ziara ya siku tano mkoani Dodoma.

*********************

Na Munir Shemweta, KONDOA

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameiagiza halmashauri ya Mji wa Kondoa kushughulikia mgogoro wa ardhi kati ya Gereza la King’ang’a na wananchi katika halmashauri hiyo.

Dkt Mabula ametoa maelekezo hayo leo tarehe 21 Septemba alipokutana na viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri za wilaya na mji wa Kondoa akiwa katika mwanzo wa ziara yake ya siku tano katika mkoa wa Dodoma.

Alisema, suala la migogoro ya mipaka linapaswa kushughulikiwa na halmashauri husika na juhudi za makusudi zisipochukuliwa basi migogoro ya ardhi haiwezi kuisha katika halmashauri.

Kwa mujibu wa Dkt Mabula, mgogoro unaoendelea sasa iwapo pande zinazopingana zingekaa pamoja na kushughulikia suala hilo ungekuwa umekwisha kwa kuwa wananchi walisharidhia kuachia sehemu ya eneo kwa shughuli za magereza.

Katika kuharakisha utatuzi wa mgogoro huo, Naibu Waziri wa Ardhi alimuelekeza Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dodoma Thadei Kabonge kupeleka wataalamu wa upimaji eneo hilo ili kuainisha mipaka na utekelezaji huo ufanyike haraka.

“Naelekeza halmashauri husika kukutanisha pande zote na kuangalia nyaraka za umiliki na utekelezaji wake ufanyike mapema ili kuondoa mgogoro huo” alisema Dkt Mabula.

Aidha, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameielekeza pia halmashauri ya Mji wa Kondoa kuhakikisha inawapatia viwanja takriban wananchi 200 katika eneo la Bicha ambapo halmashauri ilishachukua fedha kwa ahadi ya kuwapatia viwanja lakini ilishindwa kutekeleza.

“Halmashauri ya mji wa Kondoa mfikirie namna ya kusolve huu mgogoro wa wananchi ambao mmeshachukua fedha kwa ajili ya kuwapatia viwanja na hapa ofisi ya Kamishna mkoa wa Dodoma katika wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba iende kupima viwanja kwa ajili ya kuwapatia wananchi” alisema Naibu Waziri wa Ardhi.

Awali Mbunge wa jimbo la Dodoma Mjini mkoani Dodoma Ally Makoa alimueleza Dkt Mabula kuwa changamoto kubwa katika jimbo lake ni mgogoro kati ya wananchi na jeshi la Magereza, mgogoro wa eneo la hifadhi pamoja na ule mgogoro wa wananchi walinaotaka kupatiwa viwanja.

Alisema, migogoro hiyo ikitatuliwa basi katika mji huo wa Kondoa hautakuwa na migogoro ya asili na itakayoibuka ni ile itakayosababishwa na watu.

—————-MWISHO———————–

NHC YAJA NA MKAKATI MKUBWA WA KUKARABATI NYUMBA ZAKE

 

Na Munir Shemweta, KONDOA

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limesema limeanza kufanya ukarabati wa nyumba zake katika maeneo mbalimbali nchini ili ziwe katika ubora.

Hayo yalibainishwa leo tarehe 21 Sept 2021 wilayani Kondoa mkoani Dodoma na Meneja wa Kitengo cha Habari na Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa Muungano Saguya  Dodoma wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula kukagua utendaji kazi wa sekta ya ardhi katika mkoa huo.

“Shirika letu la NHC lilianzishwa mwaka 1964 na sasa tumeanza kuzifanyia ukarabati  nyumba zetu katika maeneo mbalimbali zikiwemo zile za Dar es Salaam ambapo kuna asilimia 60 ya nyumba zote za shirika” alisema Saguya

Kwa mujibu wa Saguya, NHC ina takriban nyumba 18,000 nchi nzima zinazotumika kwa shughuli za biashara na makazi na ukarabati unaofanyika utasaidia nyumba hizo kuwa na ubora na muonekano mzuri wa kuvutia.

Hata hivyo, Meneja  huyo wa Kitengo cha Habari na uhusiano NHC aliongeza kuwa, pamoja na ukarabati wa nyumba zake unaoendelea  shirika la NHC linadai takriban shilingi  bilioni 26 kutoka kwa wapangaji wake na kuwataka wote wanaodaiwa kuhakikisha wanalipa madeni yao kwa wakati ili fedha hizo zitumike kuendesha miradi mingine ya Shirika.

Saguya alibainisha kwa kusema, Shirika la Nyumba la Taifa, kwa sasa linaendelea na miradi yake ya ujenzi wa nyumba za kuuza na zile za kupangisha kwenye mkoa wa Dodoma na sasa linakamilisha mradi wa nyumba 300 eneo la Iyumbu na nyumba 100 eneo la Chamwino.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula alisema, katika kuwezesha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kabla kuanza ujenzi shirika la  nyumba linatakiwa kufanya mawasiliano na taasisi kama TARURA, Maji na TANESCO ili   kusaidia uwezeshaji miundo mbinu katika eneo la mradi.

Alibainisha kuwa, NHC kwa sasa inajenga nyumba kwa wanaohitaji kulingana na chaguo la mteja hivyo ni fursa kwa halmashauri kulitumia shirika katika miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages