Mfanyabiashara na muwekezaji wa Simba SC Mo Dewji ambaye anamiliki 49% ya hisa za Simba SC kwa thamani ya Tsh Bilioni 20 leo ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake uenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba SC na nafasi yake itachukuliwa na aliyekuwa makamu wake Salim Abdallah (Try Again).
“Mmetuunga mkono kwa miaka minne ya uongozi wangu kama Mwenyekiti wa Bodi, kwenye miaka minne tumepata mafanikio makubwa tumeshinda Ligi mara 4 na kufanya vizuri kwenye Champignons League muda umefika kama Mohammed na tumekubaliana mimi nitajiuzulu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Simba SC naomba sana msifikie kuwa mimi nimeondoka Simba bali bado ni muwekezaji”
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇