LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 22, 2021

WAZIRI MKUMBO AITAKA TANTRADE KUWA NA KITUO KINACHOTOA TAARIFA SAHIHI ZA KIBIASHARA

 


 

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof Kitila Mkumbo  ameitaka Mamlaka ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuwa kituo cha kibiashara kinachotoa taarifa, takwimu sahihi na huduma bora za kibiashara ndani na nje ya nchi ili kukuza na kuendeleza Biashara nchini.
Waziri Mkumbo aliyasema hayo katika hafla fupi ya uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANTRADE iliyofanyika Agosti 21, 2021, Makao Makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es salaam.
Akizindua Bodi hiyo, Prof Mkumbo aliitaka bodi hiyo kusimamia ipasavyo majukumu muhimu ya TANTRADE ikiwemo kuanzisha kanzi data yenye taarifa za kibiashara na kufanya utafiti ili kujua ni bidhaa gani zinazalishwa kwa wingi nchini, kuna upungufu wa bidhaa gani na bidhaa gani zinahitajika zaidi nje ya nchi.
“ Nataka kuona TANTRADE inakuwa kimbilio kwa wanyabiashara katika kuwaunganisha wazalishaji, wasindikaji wafanyabiashara kutoka maeneo ya uzalishaji na walipo wtateja wa bidhaa zao ndani na nje ya nchi kwa kutoa taarifa na takwimu sahihi pamoja na huduma bora za kibiashara”. Alisema Waziri Mkumbo.
Waziri Mkumbo pia ameitaka Bodi hiyo kuhakikisha TANTRADE inaongeza ubunifu katika matumizi ya mifumo mbalimbali ya kimtandao ya biashara inayolenga kuongeza upatikanaji wa taarifa mbalimbali za kibiashara kwa urahisi ili kuwezesha upatikanaji wa masoko ndani na nje ya nchi kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini.
Bodi hii pia inatakiwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali pamoja na sekta binafsi katika kuelimisha na kuhamasisha uboreshaji wa bidhaa zinazozalishwa nchini, upatikanaji wa masoko, uendeshaji wa biashara, kujenga uelewa juu ya usafirishaji wa bidhaa hizo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati ili kufikia soko la ndani, kikanda na kimataifa. Alisema Prof. Mkumbo
Aidha, Prof. Mkumbo pia ameielekeza Bodi hiyo kutekeleza jukumu la msingi la Bodi katika kutengeneza mkakati wa kufikia malengo ya Taasisi na kusimamia utekelezaji wake kwa kutoa ushauri ndani na nje ya vikao vya Bodi, kuwa mtunza nidhamu wa Mkuu na Menejimenti ya Taasisi kwa niaba ya Mmiliki na kutoa au kushauri katika kutatua changamoto za kimenejimenti huku ikizingatia kutokufanya kazi za menejimenti.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages