Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), Titus Kaguo akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa Kanda ya Kati wa kuelezea majukumu, mafanikio na changamoto ya mamlaka hiyo, jijini Dodoma leo.
Sehemu za wandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo wa kuwajengea uelewa wa majukumu, mafanikio na changamoto ya mamlaka hiyo.
Wito huo umetolewa na Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa EWURA, Titus Kaguo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa Kanda ya Kati wa kuelezea majukumu, Mafanikio na Changamoto ya mamlaka hiyo, jijini Dodoma leo.
Amesema kuwa EWURA ambayo imepewa mamlaka ya kusajiri kampuni na wafanyabiashara watakaoingia mikataba ya kutoa huduma wakati wa ujenyi wa bomba hilo, hadi sasa kampuni ya kitanzania zilizojisajili ni 776 wakati Uganda tayari wamejisajiri 4000.
Ameviomba vyombo vya habari kusaidia kuhamasisha watanzania wajitokeze kwa wingi kwenda kujisajili na kwamba masharti siyo magumu, ili mradi wafuate sheria kwa kuwa na kampuni iliyosajiliwa kihalali.
Amesema kuwa itakuwa vigumu kupata tenda kwenye mradi huo mpaka ujisajili EWURA.
Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
0754264203
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇