LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 13, 2021

WAFANYA BIASHARA MKOA WA MWANZA WAPATA UONGOZI MPYA

    Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

Wafanyabiashara Mkoa wa Mwanza wamefanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali katika chama chao cha chemba ya biashara ,viwanda na kilimo mkoani hapa kutokana na katiba inayowaongoza.

Mwenyekiti mpya wa chama cha chemba cha wafanyabiashara,viwanda na kilimo(Tccia) Gabriel kenene alisema mambo ambayo amepanga kuyafanya katika uongozi wake nikuimarisha chemba za wilaya na kutatua changamoto zinazowakabili,kuwatetea wafanyabiashara pamoja na kupata Wanachama wampya.

Amesema pamoja na changamoto zinazowakabili watajitahidi  kutoa elimu na kuhakikisha kila sekta ya serikali inayofanya kazii za wafanyabiashara hao kujenga mawasiliano mazuri ili kuweza kutatua matatizo yanayowakabili na ikiwa na kujenga mahusiana  mazuri ilikuweza ukaribu wa kufanya shuguli za kiuchumi kwa njia ya vikao vya mara kwa mara amesema Kanena.

Naye makamu mwenyekiti upande wa viwanda Mwanabure Ihuya alisema atasimama imara kwa lengo la kufanya kazi ilikuwawakilisha vyema wanawake na Wanachama kwa ujumla ilikuweza kutimiza ndoto.

Ihuya amesema kupitia njia ya uelimishaji watawainua wanawake iliwaweze kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika sekta za viwanda ilikujiinua kiuchumi na kufikia hatua ya ushindani kibiashara.

Kwa upande wake makamu  wa rais wa Tccia Joseph Kahungwa alisema Wanachama na wasio

wanachama wananufaika kupitia chemba hiyo kwa shuguli za kiuchumi kupitia mafunzo ya ujasiliamali,uwakilishi huainisha changamoto na kuziwasirisha sehemu husika.

Kahungwa alisema mafanikio ni makubwa katika chemba ya wafanyabiashara wameboresha sera mbalimbali serikali imesikia na imeondoa tozo nyingi ambazo zilikuwa siyo rafiki kwa wafanyabiashara na imeweka mfumo wa mawasiliano mazuri.

Ametoa wito kwa wafanyabiashara ambao hawajajiunga wajiunge iliwaweze kunufaika kupitia chemba hiyo kwa shuguli zao za kiuchumi na taifa kwa ujumla.

Na  miongoni mwa nafasi ambazo ziepata viongozi hao ni uongozi Mwenyekiti Mkoa wa Mwanza,makamu mwenyekiti biashara,makamu mwenyekiti viwanda,makamu mwenyekiti kilimo na wajumbe wa halmashauri kuu Mwanza.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages