LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 4, 2021

VIONGOZI WA DINI, VYAMA VYA SIASA DODOMA WAPIGWA MSASA KUHUSU CHANJO YA CORONA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akifafanua jambo  kuhusu umuhimu wa wananchi kupata chanjo wakati wa kikao na  viongozi wa dini, vyama vya siasa,  mabaraza ya wazee na viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu  ya kuwajengea uwezo kuhusu faida na madhira ya chanjo ya Corona jijini Dodoma leo Julai 4,2021. Kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Fatma Mganga.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt Fatma Mganga., akijibu baadhi ya hoja kutoka kwa vingozi walihudhuria kikao hicho, likiwemo suala la viongozi wa dini kuendelea na maombi na toba kuitokomeza Corona.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjinu, Meja Mstaafu Johnick Risasi akielezea alivyochanjwa chanjo ya Corona jana na kutoa ushuhuda kuwa hajapata madhara, hivyo kuwataka viongozi kuwa mfano  kuwa wa kwanza kwenda kuchanja. 

 Kiongozi wa Maknisa Mkoa wa Dodoma, akiomba  Mungu kufanikisha kikao hicho muhimu kwa viongozi wa dini na wengineo.

Mwakilishi wa  Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, akiuombea dua mkutano huo.


Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM Mkoa wa Dodoma, Peter Mavunde akielezea kuhusu hatari ya ugonjwa Corona amabao hata yeye ulimpata.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Samuel Seseja akijibu hoja mbalimbali za viongozi wa dini na vyama vya siasa kuhusu  faida na madhira ya chanjo ya Corona ambapo alisema kuwa iko salama imethibitishwa na watalaamu hapa nchini.
Sehemu ya viongozi wa dini na wanasiasa pamoja na wazee wakiwa katika kikao hicho.



Afisa Afya wa Mkowa Dodoma,  akionesha sanitaiza amabayo ni moja ya kinga ya maambukizi ya Corona.



PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA



Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma

Viongozi wa dini wameshauriwa kwenda kuwapatia waumini wao   Elimu juu ya umuhimu wa chanjo ya Corona.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Anthony Mtaka wakati wa kuhitimisha kikao chake na viongozi  alolihokiitisha kuwajengea uwezo kuhusu faida ya chanjo hiyo iliyozinduliwa jana mkoani humo.

Licha kikao hicho kuhudhuriwa na viongozi wa dini, kiliwashirikisha pia viongozi wa vyama vya siasa,  mabaraza ya wazee na viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu kutoka Wilaya za Mkoa huo.

"Hatuwashawishi kwenda kupata chanjo, bali mnatakiwa muwapelekee waumini wenu elimu sahihi mliyoipata hapa kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo ya Corona na kuwaacha waamue wenyewe kwa hiari kuchanjwa," amesema Rc Mtaka

Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Samuel Seseja aliwatoa hofu viongozi hao kuhusu usalama wa chanjo hiyo ya Corona ambapo pia alikiri kuwa madhira madodo madogo kama ilivyo hata kwa chanzo za magonjwa mengine.

Ili wapate uelewa mzuri wa kuweza kwenda kuwaelimisha waumini wao, viongozi walipata wasaa wa kuhoji mambo mbalimbali ikiwemo kutaka kujua ubora wa chanjo hiyo Janssen kutoka Marekani.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Mganga amewataka viongozi wa dini kuendelea kutoa maombi na toba kwa waumini ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya hilo la Corona.

Aidha, Dkt Mganga amesema kuwa katika mapambano dhidi ya janga hili la Corona inabidi kutumia silaha zote kupambana  nalo ikiwemo kupigwa chanjo, maombi, lakini pia hawazuiwi kutumia  tiba zingine  walizozizoea kama vile kujifukiza,kutumia malimau, tangawizi na dawa zingine za asili zinazofaa.

Baada ya viongozi wengi kujiridhisha na elimu waliyoipata juu ya chanjo hiyo, walimuomba RC Mtaka kuwaandalia utaratibu wa kwenda kupata chanjo, ombi ambalo alilikubali.

Baadhi ya viongozi waliomba kupewa muda wa kwenda kuwaelimisha  waumini wao juu ya elimu hiyo ya chanjo ya Corona.

Mkoa wa Dodoma umepata dozi 50,000 za chanjo ya Corona aina ya Janssen kutoka Marekani ambapo uzinduzi ulifanyika jana Julai 3,2021 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Makundi yaliyopewa kipaumbele ni wahudumu wa sekta ya afya, wazee wenye umri kuanzia miaka 50 pamoja na watu wenye magonjwa sugu kama vile pumu, athma, presha na kisukari.







No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages