LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 19, 2021

Video: VIONGOZI CCM DODOMA WAHAMASISHA WANAWAKE KUJITOKEZA KUPATA CHANJO

 VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dodoma wamejitokeza kuhamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kwenda kupata chanjo ya Corona kwa usalama wa afya zao na za wengine.

Hamasa hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti baada ya kushiriki chanjo katika Kituo cha Afya cha Makore Dodoma Mjini, ambapo viongozi hao walipata chanjo pamoja na akina mama wengine waliojitokeza. Walioongoza katika uhamasishaji huo ni Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbanga, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Mkoa wa Dodoma, Neema Majule ambaye alionesha kadi ya chanjo aliyopatiwa baada ya kuchanjwa siku ya uzinduzi mkoani humo, Katibu wa UWT wa Mkoa huo, Mariam Kireti., Diwani wa Viti Maalumu Wilaya ya Dodoma Mjini, Joice King pamoja na wanachama wengine wa chama hicho. Mdau nakuomba uendelee kusikiliza hamasa walizotoa viongozi hao kupitia clip hii ya video. Imeandaliwa na Richard Mwaikenda
 Mhariri Blog ya Taifa ya CCM
 0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages