LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 17, 2021

TAARIFA KUTOKA IKULU MDA HUU

Rais Samia Suluhu Hassan


Ikulu, leo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali  kama ifuatavyo:-

1. Amemteua Jaji Mstaafu Mohamed Chande Othman kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).


2. Amemteua Prof.  Elisante Ole Gabriel kuwa Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.  Kabla ya uteuzi huu Prof. Ole Gabriel alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (upande wa Mifugo) na anachukua nafasi ya .Mathias Kabunduguru ambaye amestaafu.  


Taaria iliyotowa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais. Ikulu leo, Jaffar Haniu, imeeleza kuwa, Prof. Ole Gabriel ataapishwa tarehe 21 Agosti, 2021, saa 03:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam pamoja na Mabalozi Wateule watatu, wafuatao:-

1. Balozi Mteule Lt. Jen. Yakub Hassan Mohamed kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Uturuki.

2. Balozi Mteule Mahmoud Thabit Kombo kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia.

3. Balozi Mteule Elsie Sia Kanza kuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages