Na Anthony Ishengoma, Shinyanga
Waziri wa Madini Doto Biteko amesema ndani ya siku 60 atafuta leseni za uchimbaji madini za wale wamiliki ambao wameodhi maeneo ya madini bila kuyafanyia kazi kwa muda mrefu lakini wamekuwa wakijitokeza kuzuia wachimbaji wadogo kutumia maeneo hayo kwa kigezo cha kumiliki leseni.
Doto Biteko amesema kuna baadhi ya watu wanaleseni nchi nzima na inapotokea wachimbaji wadogo wakagundua eneo hilo lina madini watu hao anajitokeza kudai tayari wana leseni za eneo hilo na kujiuliza mtu huyo muda wote anakuwa wapi.
Kufuatia hali hiyo Biteko amesema sio tu kwamba atafuta leseni zinazomolikiwa kwa kipindi kirefu bali pia atahakikisha wamiliki hao wanalipa kodi ya serikali kwani mpaka sasa serikali inadai jumla ya Tsh Bil.9 ambazo amesema lazima zilipwe kwa serikali kutoka kwa wamiliki hao.
Biteko amesema hayo jana wakati wa akifunga Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini ambayo yamefanyika kwa takribani wiki moja sasa na kuongeza kuwa anashangaa kuwa bado kuna watanzania wanaangaika kutorosha madinio nje ya Nchi.
Biteko amewataka watanzania kuwa wazalendo kwa kulipa kodi ya serikali badala ya kutorosha madini kwani Tanzania ina masoko ya madini 50 hapa nchini na kuna wafanyabiashara ya madini kutoka Congo ambao wanekuwa wakifika Tanzania kwa ajili ya kuuza madini uku akisema kuwa kutorosha madini ni sawa na kuchoma kuni kwa kutumia mwanga wa tochi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kwa upande wake amesema yuko tayari kupambana na watoroshaji madini hao na kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja kwani ikiwa watabainika atahakikisha wanafirisika na kutaifisha madijni yote watakayokuwa nayo.
Dk. Sengati amewataka watanzania kutanguliza uzalendo mbele kwa ustawi wa uchumi wa wana Shinyanga na watanzania kwa ujumla na kwamba atakuwa mkali sana kwa wale wote ambao wataendelea na ukosefu wa uzalendo kwa kuendelea kutolosha madini hapa Nchini.
Naye Mwenyekiti wa Tume ya madini nchini Prof. Idris Kikula ameongeza kuwa serikali inalazimika kufuta leseni izo ndani ya siku sitini zijazo huku akijua maamuzi hayo hayatawafuraisha watu lakini hamna namna lazima uamzi huo ufanyike na kodi izo zilipwe kwa manufaa ya Taifa.
Prof. Kikula ameongeza kuwa kuhusu suala hilo tayari Tume ya madini imeshatoa tangazo ikiwemo mikutano ya vyombo vya habari na kuwataka wamiliki waleseni hizo kuwa tayari na zoezi hilo na kuwataka kuwa tayari kulipa kodi inayodaiwa na serikali.
Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya madini yamefanyika katika viwanja vya Zainab Telack nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga na yamehitimishwa jana na yanatarajia kuendelea tena mwakani kwa kipindi kama hiki ili kutoa fursa kwa wananchi kujua soko la madini lakini pia kujipatia elimu ya teknolojia ya madini.
Waziri wa Madini Doto Biteko akikagua madini aina ya Almasi alipotembelea banda lenye madini hayo wakati wa kufunga Maonesho ya Biashara na Teknolijia ya Madini jana Mkoani Shinyanga.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇