LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 6, 2021

RAIS SAMIA AONGOZA KUAGWA MWILI WA KUANDIKWA, ASEMA SERIKALI IMEMPOTEZA MTUMISHI NA KIONGOZI MWADILIFU, MAKINI, SHUPAVU NA MCHAPAKAZI

Karimjee, Dar es Salaam

Rais Samia Sluluhu Hassan amesema kifo cha aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  Elias Kwandikwa,kimeacha simanzi na pengo kubwa si kwa familia pekee bali pia kwa Serikali na Taifa kwa ujumla na kuongeza kuwa kufuatia kifo hicho Serikali imempoteza mtumishi na kiongozi mwadilifu, makini, shupavu na mchapakazi hodari. 


Rais Samia ameyasema hayo wakati akitoa salamu za pole wakati akiwaongoza viongozi mbalimbali na waombolezaji kuaga mwili wa Marehemu Elias Kwandikwa katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam, leo.


Aidha  Rais Samia amewashukuru viongozi wa dini kwa kuongoza ibada ya kumuaga marehemu Kwandikwa ambapo mahubiri yao yametoa faraja na kukumbusha kuwa wanadamu duniani wanapita, hivyo kutakiwa kuishi kwa wema na kutenda yale ya kumpendeza Mungu.


Shughuli za kuaga mwili wa Marehemu Kwandikwa zimekuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, Rais wa Zanzibar Dk. Hussein Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdallah, Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson, Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga, Katibu Mkuu Kiongozi-Zanzibar Mhandisi Zena Said  na viongozi wengine wa  vyama vya Siasa na Serikali.  

Rais Samia Suluhu Hassan, akiongoza Viongozi mbalimbali na Wananchi  kuaga Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  marehemu  Elias John Kwandikwa katika Viwanja vya Karimjee  Jijini Dar es Salaam leo

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages