LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 6, 2021

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI , LEO

Rais Samia Suluhu Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 06 Agosti, 2021 amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:-

1.      Amemteua Bw. Athumani Seleman Mbuttuka kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali (Internal Auditor General).

Bw. Mbuttuka anachukua nafasi ya Balozi Mohamed Mtonga ambaye amestaafu na Balozi wa Tanzania katika Falme za Kiarab. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Mbuttuka alikuwa Msajili wa Hazina (Treasury Registrar).

2. Amemteua Bw. Leonard John Mkude kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali (Accountant General). Bw. Mkude anachukua nafasi ya Bw. Francis M. Mwakapalila ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi, Bw. Mkude alikuwa Meneja Bajeti, Benki Kuu ya Tanzania.

3. Amemteua Bw. Mgonya A. Benedict kuwa Msajili wa Hazina.

Bw. Benedict anachukua nafasi ya Bw. Athumani Mbuttuka ambaye ameteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali. Kabla ya uteuzi huo, Bw. Benedict alikuwa Meneja wa Masuala ya Fedha na Madeni, Benki Kuu ya Tanzania.

4. Amemteua Bw. Frank Mugeta Nyabundege kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (Tanzania Agriculture Development Bank). Kabla ya uteuzi huo, Bw. Nyabundege alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Lake Oil Tanzania Limited.

5. Amemteua Bw. Casmir Kyuki kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS. Bw. Kyuki ni Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Teuzi hizi zimeanza tarehe 05 Agosti, 2021.

Jaffar Haniu

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages