Iringa, leo
Mwenyekiti wa Kampuni za Asas Group, Alhaj Faraj Ahmed Abri ambaye ni Baba mzazi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Salim Abri Asas amefariki dunia leo Ijumaa Agosti 13 alfajiri, akiwa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika familia hiyo, Mzee Abri , maziko yake yatafanyika leo baada ya Swalat Adhuhuri katika Makaburi ya Kisutu Dar es Salaam.
"Hakutakuwa na mikusanyiko kwa tutakaokuwa Iringa, tafadhali tutumie zaidi teknolojia za habari kutoa pole na shughuli nyingine," ilieleza taarifa hiyo.
Mwenyekiti wa CCM, Manispaa ya Iringa Said Rubeya alithibitisha taarifa hiyo na kutoa pole kwa familia, wafanyakazi wa Asas, ndugu jamaa na marafiki.
"Kama tulivyo shauriwa tutumie teknolojia ya habari na mawasiliano kuomboleza, nitoe pole nyingi kwa familia, pole pia kwa M NEC wetu, Salim Asas. Hakika kwa Mwenyezi Mungu ni marejeo," alisema Rubeya.
SORCE: Mwananchi Online
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇