LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 6, 2021

MSIGWA AWATAKA MAAFISA UHUSIANO KUTOA TAARIFA SAHIHI KWA JAMII KUEPUSHA UPOTOSHAJI


Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza katika mkutano na Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Serikalini,Wizara, Mashirika na Taasisi jijini Dodoma leo Agosti 6,2021, ambapo amewataka  kuwa vinara katika kuhakikisha Wananchi wanapata taarifa sahihi  ili kuondoa  changamito ya upotishaji inayoendelea katika jamii na kuleta hofu.
Baadhi ya maafisa hao wakisikiliza kwa makini wakati, Msigwa akizungumza nao.



 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA



Na Dotto Kwilasa, Dodoma.

MSEMAJI Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amewataka Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Serikalini,Wizara, Mashirika na Taasisi kuwa vinara katika kuhakikisha Wananchi wanapata taarifa sahihi  ili kuondoa  changamito ya upotishaji inayoendelea katika jamii na kuleta hofu.

Msigwa ameyasema hayo jana Jijini hapa kwenye kikao kazi kati yake  Maafisa hao huku akiwataka kuwa wepesi kuisemea Serikali Kwenye maeneo yao na kuepusha taarifa za upotoshaji .

Alisema,licha ya tatizo la upotoshaji wa taarifa kuwepo tangu mwanzo,kwa Sasa  limezidi na kupelekea kukwamisha baadhi ya shughuli za maendeo hivyo kuwataka Maafisa uhusiano kufanya kazi kwa weledi na wakati ili kuondoa changamoto hiyo.
 
"Lazima tutimize majukumu yetu kwa kuwa vinara kuhakikisha watu wanapata taarifa sahihi kuihusu Serikali,linapotokea tatizo kama hilo sisi ndio tunaopaswa kuwajibika kuisemea Serikali,tusisubiri mambo yaharibike,"alisema .

Mbali na hayo aliwataka pia kuongeza juhudi katika utendaji kazi na kamwe wasiruhusu wananchi kupotoshwa.

" Katika utendaji kazi wenu msikubali kuruhusu kutolewa taarifa za uongo,kumbukeni kuwa vyanzo vya taarifa ni nyinyi naomba hili jambo mlifanyie kazi kwa weledi na  nguvu zote,"alisisitiza.

ATAKA  KIPAUMBELE VYOMBO VYA HA BARI ZA KIJAMII.

Katika hili,Msemaji huyo wa Serikali ametaka Maafisa Uhusiano na  Mawasiliano Serikalini kutopuuza vyombo vya habari vya Kijamii na kusema kuwa haipendezi kuvibagua kwa kuwa navyo vina umuhimu sawa na vyombo vingine.

"Msivipuuze vyombo vya habari za kijamii lazima  tushirikiane navyo haipendezi wewe ni Afisa habari wa Taasisi fulani alafu unabagua vyombo hivi kana kwamba havifai ,"alisema na kuongeza;

"Lazima mtambue kuwa vyombo hivi vimesajiliwa  ili vitumiwe kutoa taarifa mbalimbali kwa jamii,vilevile vyombo hivi hivi mnavyovidharau endapo mtavitumia  vitawapa muda wa kutosha kukanusha masuala ya upotoshaji kwa jamii kwa Kuwa ndiyo vipo karibu zaidi na jamii,"

MITANDAO YA KIJAMII

Kuhusu mitandao ya kijamii Msigwa aliwataka Maafisa hao kutumia Mitandao vizuri linapokuja suala la akauti za Wizara huku alisisitiza kuwa kuna ulazima wa kuzofanyia kazi Mara kwa  mara akaunti hizo na kuleta maana iliyokusudiwa  .

"Siamini kwamba siku inaweza kuisha bila kuwa na jambo  la kuitaarifu jamii ,wewe usipotumia mtu mwingine ataitumia nafasi hiyo kupotosha,Tovuti za Serikali lazima ziwe hai  kufikia lengo la kuhakikisha watanzania wanapata taarifa sahihi,"alisema na kuongeza;

"Tunapotekeleza majukumu yetu kuna njia nyingi za kufikisha taarifa,nitoe wito kwa vyombo vya habari za kijamii kuzingatia masuala ya utoaji wa taarifa sahihi,"alisisitiza.

Msigwa pia aliweka sawa kwenye tatizo la upotoshaji na kusema kwamba sio vyombo vya habari ndivyo vinafanya upotoshaji huo bali ni Mitandao ya kijamii hivyo jamii inapaswa kuwa macho kuelewa usahihi wa habari.


No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages