Na Jastin Cosmas Kibondo
Mbunge wa jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Dk. Frolence Samizi amewataka wananchi kuhakikisha wanaanzisha Benki ya Matofali, ili kuweza kuongeza vyumba vya madarasa katika shule za msingi na sekondari.
Kauli hiyo ameitoa wakati alipokuwa anazungumza na wananchi wa kijiji cha Kitahana, kata ya Kitahana hapa wilayani Kibondo, ambapo amewaasa wananchi kushiriki katika ujenzi wa Taifa,ili kuondokana na changamoto zinazo wakabili.
Jimbo la Muhambwe lina jumla ya kata 19, huku kata 5 zikiwa zinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa shule za Sekondari.
Kata ya Kitahana, ni miongoni mwa kata ambazo zinakabiliwa na changamoto hiyo ambapo mbunge ametoa rai kwa viongozi wa kata hiyo kwa kushirikiana na wananchi, kuhakikisha wanashiriki shughuli za maendeleo.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kitahana, Christopha Sindalusize amemhakikishia mbunge wa jimbo la muhambwe kuwa, jitihada za kumalizia vyumba vya madarasa zitafanyika, ili wanafunzi waanze masomo ifikapo mwakani.
Mbunge wa jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Dk Frolence Samizi akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kitahana jimboni humo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇