LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 24, 2021

MBOWE NA WENZAKE WASOMEWA MASHTAKA SITA LEO, LIMO LA KUTAKA KUMDHIRU OLE SABAYA

Kisutu, Dar es Salaam

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Ilala mkoani Dar es Salaam, leo imewasomea mashtaka sita Mwenyekiti wa chama cha Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu, likiwemo la kutaka kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya.


Mbali na Mbowe wengine kwenye kesi hiyo ni waliokuwa Walinzi wake, Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa na Mohamed Abdallah Ling'wenya.


Mashitaka hayo yamesomwa na upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga akisaidiana na Ester Martin, wakati wakiwasomea washtakiwa hao wamaelezo ya mashaidi na vielelezo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.


Inadaiwa Mbowe alituma kiasi cha sh. 600,000 kwa washitakiwa wenzake kwa ajili ya kufanya maandalizi ya vitendo vya ugaidi ikiwemo kutaka kulipua vituo vya mafuta, mikusanyiko ya watu, kukata miti na kuisambaza barabarani.


Mashtaka hayo ni pamoja na kula njama za kutenda ugaidi ambapo Mbowe anatuhumiwa kufadhili vitendo hivyo vya kulipua vituo vya mafuta kwa kutoa zaidi ya sh. 600,000.


Pia washitakiwa wote wanatuhumiwa kushiriki vikao vya kutenda kosa la ugaidi huku mshtakiwa wa pili akituhumiwa kumiliki bastola na risasi tatu kwa ajili ya kutenda kosa la ugaidi.


Mshtakiwa wa kwanza anatuhumiwa kumiliki nguo, begi na koti zote za Jeshi la Wananchi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).


Aidha, mashahidi 24 na vielelezo 19, wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi inayomkabil Mwenyekiti huyo wa Chadema na wenzake watatu.


Miongoni mwa mashahidi hao ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai nchini, DCI Robert Boaz.


Mbowe

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages