LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 10, 2021

MASHINDANO YA MAJESHI YARINDIMA DODOMA

Wachezaji wa Timu ya Polisi (waliovaa jezi nyeusi) wakichuana na timu ya Magereza (waliovaa jezi ya njano) katika mchezo wa mpira wa kikapu wakati wa mashindano ya Majeshi yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya John Merlini jijini Dodoma.Mashindano hayo yamedhaminiwa na Kampuni ya Silent Ocean.



Wachezaji wa timu ya Magereza wakichuana na timu ya Polisi katika mchezao wa soka wakati wa mashindano ya Majeshi yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya John Merlini jijini Dodoma.



Wachezaji wa timu ya JKT Mbweni (waliovaa bluu bahari) wakichuana na timu ya Polisi (waliovaa njano) katika mchezo wa mpira wa pete wakati wa Mashindano ya Majeshi yanayoendelea kwenye viwanja vya Shule ya John Merlini jijini Dodoma.






Wachezaji wa timu ya majeshi kutoka Zanzibar wakifanya mazoezi ya  mpira wa wavu.
Baadhi ya viongozi wa mashindano hayo  wakiwa na maofisa kutoka kampuni ya Silent Ocean iliyodhamini mashindano hayo.
Wachezaji wa timu ya soka ya Polisi wakitoka uwanja wakati wa mapumziko katika pambano lao dhidi ya Magereza kwenye viwanja vya Shule ya John Merlini, Dodoma.


 Kikosi cha timu ya soka ya Polisi kikiwa kimevalia jezi iliyotolewa na wadhamini Sileny Ocean.


Imeandaliwa na Richard Mwaikenda

Mhariri Blog ya Taifa ya CCM

0754264203

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages