LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 10, 2021

KATIBU MKUU WA CCM DANIEL CHONGOLO ATOA SIKU 14 KWA VIONGOZI WA CCM NGAZI ZOTE NCHINI KUWASILISHA MAKAO MAKUU TAARIFA YA UKAGUZI WA MIRADI INAYOENDELEA KATIKA MAENEO YAO

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, leo ameongoza Seketarieti ya CCM kufanya ziara ya ukaguzi wa reli ya Kisasa ya Mwendokasi (SGR) Kilosa mkoani Morogoro na kutoa siku 14 kwa viongozi wa CCM katika ngazi zote nchini kuwasilisha katika Makao Makuu ya CCM taarifa ya ukaguzi wa Chama katika miradi inayoendelea kufanyika katika maeneo yao.


"Uwepo wangu na Sekretarieti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika ukaguzi wa reli hii ya mwendokasi ikawe salamu kwa uongozi wa mikoa, wilaya, kata na matawi yote nchini kufanya ukaguzi wa miradi inayoendelea kufanyika katika maeneo yao na kuleta taarifa ya miezi sita kwetu ili tuone utekelezaji wa ilani ya CCM 2020 -2025 unavyotekelezwa", amesema Chongolo na kuongeza;


"Ripoti ya miezi sita itakayoletwa kwetu ikitokea ngazi ya Matawi, Kata, Wilaya hadi mkoa itatupa mwangaza wa kujua ni kwa jinsi gani serikali iliyopo madarakani iliyosimamiwa na CCM inatekelezaje Ilani ya Chama chetu".


Chongolo kwa niaba ya Sekreterieti ya CCM, alitoa pongezi kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mkandarasi wa ujenzi wa Reli hiyo ya SGRu Yapi Merkez na Serikali kwa ushirikiano mzuri unaoonekana katika ujenzi wa reli hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na Mjumbe wa Kamati ya Siasa wa CCM wa mkoa huo, Martin Shigela ambaye alikuwa katika ziara hiyo, alisema, Serikali ya Mkoa wa Morogoro wanawashukuru viongozi wa CCM Taifa wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama, Chongolo kwa kutembelea mradi huo na kuona kinachoendelea saiti.


"Kwa niaba ya serikali ya Mkoa wa Morogoro tunawashukuru viongozi wetu wa Kitaifa wa CCM kutembelea leo mradi huu wa ujenzi wa reli ya mwendokasi, sisi kama serikali kila siku jukumu letu ni kuhakikisha Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inatekelezwa kwa asilimia 100% katika mkoa wetu;


Pia serikali ya mkoa wa Morogoro tunawashukuru viongozi wa Shirika la Reli Nchini (TRC) na Mkandarasi wa ujenzi wa reli hii ya mwendokasi (Yapi Merkez) kwa kutupa ushirikiano wa kutosha ilipotokea ajali ya treni kwa kutoa magari tuliyosafirishia wahanga wa ajali ile kuelekea hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro", alisema Shigela.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, alimshukuru Katibu Mkuu wa CCM,o na Sekretarieti yake kutembelea mradi huo, akisema hatua hiyo wao kama shirika inawapatia hamasa ya kuona Serikali na Chama wapo pamoja nao na kuwazidishia hamasa ya kushirikiana vyema na mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akizungumza wakati wa ziara yake na Sekretarieti kukagua mradi wa Reli ya Treni ya Mwendokasi (SGR) Kilosa mkoani Morogoro, leo.


 





No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages