Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KATA ya IFULIFU ni moja ya Kata 21 za Jimbo la Musoma Vijijini. Ni hii Kata pekee ambayo haina Shule yake ya Sekondari.
KATA hii inaundwa na Vijiji 3, ambavyo ni Kabegi, Kiemba na Nyasaungu.
Wanafunzi wa Sekondari wanaotoka kwenye Kata hii
wanalazamika kutembea umbali mrefu kwenda masomoni kwenye Sekondari za
Kata za jirani ambazo ni Kata ya Mugango (Mugango Sekondari) na Kata ya
Nyakatende (Nyakatende Sekondari).
WANAVIJIJI wa Kata hii wameamua kujenga Sekondari Mbili (2) kwa utaratibu huu:
*Kijiji cha Nyasaungu, kinajenga Sekondari yake kwa kushirikiana na Mbunge wao wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo
*Vijiji vya Kabegi na Kiemba, nao wanajenga Sekondari yao kwa kushirikiana na Mbunge wao wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo
NYASAUNGU SEKONDARI YA KIJIJI CHA NYASAUNGU
MWENYEKITI wa Serikali ya Kijiji cha Nyasaungu, Ndugu
Magesa Chacha ameeleza kuwa, Ujenzi wa Sekondari yao ulianza JULAI 2019
na malengo yao ni NYASAUNGU SEKONDARI ifunguliwe mwakani (Januari 2022).
Mbali ya umbali mrefu wa kilomita 24 za watoto wao
kutembea kwenda masomoni Mugango Sekondari, WANAFUNZI wa KIKE
wanapambana na vishawishi vingi na baadhi kupata mimba na kukatisha
masomo yao.
MIUNDOMBINU INAYOJENGWA
*Vyumba 2 vya Madarasa na Ofisi 1 tayari vimeishaezekwa
*Choo chenye Matundu 6, tayari kimeishaezekwa.
*Jengo la Utawala (msingi unachimbwa, na ujenzi utaanza hivi karibuni)
*Maabara 3 zitajengwa
*Maktaba itajengwa
*Nyumba za Walimu zitajengwa
MAKUNDI YANAYOCHANGIA UJENZI WA NYASAUNGU SEKONDARI
*Michango ya Kijiji cha Nyasaungu ni endelevu kulingana na mahitaji ya MIRADI ya MAENDELEO ya Kijiji hicho.
(i) Kaya zenye ng’ombe zaidi ya 100, michango yao ni Tshs 200,000 (Laki mbili)
(ii) Kaya zenye ng’ombe 99-50, michango yao ni Tshs 100,000 (Laki moja)
(iii) Kaya zenye ng’ombe chini ya 50, michango yao ni Tsh. 40,000 (elfu arobaini)
(iv) NGUVUKAZI za Wanakijiji za kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji ya ujenzi.
(v) Michango ya MBUNGE wa JIMBO Profesa Sospeter Muhongo:
*Mabati 108
*Saruji Mifuko 35
*Nondo 20
MFUKO wa JIMBO
*Mabati 54
*Saruji Mifuko 80
WANAKIJIJI na VIONGOZI wao kwa kipekee kabisa, wanatoa
shukrani nyingi sana kwa MBUNGE wao wa JIMBO, Mhe Prof Sospeter Muhongo
kwa jitihada kubwa anazoziweka kwenye UTEKELEZAJI wa MIRADI ya MAENDELEO
ya Kijiji chao – amechangia madawati na vitabu kwenye Shule yao ya
Msingi. AMEFUFUA na kuchangia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji chao.
OMBI KUTOKA KIJIJI CHA NYASAUNGU
WAZALIWA wa Kijiji cha Nyasaungu, na Kata nzima ya
Ifulifu wanaombwa kutoa MICHANGO kwenye ujenzi wa Nyasaungu Sekondari
ambayo itapokea Wanafunzi kutoka Kata yao na Kata za jirani.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇