Meneja Urasimashaji Biashara wa MKURABITA,Hancy Kombe akichokoza mada wakati wa kikao hicho. |
Kikao kikendelea
Afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) Dodoma, Ezekiel Emmanuel akichangia mada wakati wa kikao hicho.
Meneja Mauzo wa Kanda wa Benki ya NMB, Ungandeka Mwakatage akielezea kuhusu vigezo vya kukopa fedha kwenye benki hiyo.
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI
YA RAIS - IKULU
MPANGO
WA KURASIMISHA
RASILIMALI
NA BIASHARA ZA WANYONGE TANZANIA
|
TAARIFA YA TATHMINI YA UTAFITI WA MSINGI
KWA BIASHARA YA BODA BODA/ BAJAJI KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA
AUGUST, 2021
YALIYOMO
1.1 Lengo la Kuanzishwa
MKURABITA
2.0 Majukumu ya wadau wa urasimishaji biashara ya bodaboda
2.1 Halmashauri ya jiji
la dodoma
2.2 Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA)
2.3 Mamlaka ya Udhibiti wa
Usafiri Ardhini (LATRA)
2.4 Polisi – Kitengo Cha Usalama
Barabarani
2. Taasisi za kifedha nI
CRDB, NMB NA EQUITY
NA AMANA BENKI
2.6 Shirika La Taifa
La Hifadhi Ya Jamii (NSSF)
2.7 Umoja Wa Madereva
Pikipiki Dodoma – UMAPIDO
3.0 Utekelezaji Wa Shughuli Za Urasimishaji Biashara Ya Boda
Boda Na Bajaji
3.1 Kazi ya Uwandani na Methodolojia
3.2 Lengo La Tathmini
Ya Utafiti Wa Msingi Kwa Waendesha Boda Boda
4.0 Matokeo Ya
Tathmini Ya Utafiti Wa Msingi Kwa Waendesha Boda Boda
4.1 Kubaini umiliki
wa boda boda na Bajaji
4.2 Kubaini upatikanaji
wa Mitaji na Mauzo kwa waendesha Boda/Bajaji
4.3 Kubaini usajili wa
biashara ya bodaboda/bajaji
4.4 Kubaini upatikanaji
wa ajira kupitia bodaboda/bajaji
4.5 Kubaini upatikanaji
wa mikopo ya bodaboda/bajaji
4.6 Kubaini upatikanaji
na uhitaji wa mafunzo ya urasimishaji
VIFUPISHO
VYA MANENO
BRELA : Wakala wa Usajili wa Biashara
MKURABITA : Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara
za
Wanyonge Tanzania
NSSF : Mfuko ya Hifadhi ya Jamii
TEHAMA : Teknolojia, Habari na Mawasiliano
TRA : Mamlaka ya Mapato Tanzania
TIN : Nambari ya Mlipa Kodi
TRA : Mamlaka ya mapato
LATRA :
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini
UMAPIDO : Umoja wa Madereva Pikipiki Dodoma
1.0 UTANGULIZI
Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na
Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)
Ilianzishwa
na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 30 Septemba, 2003 kwa
Tamko la Rais wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin William Mkapa.
Utekelezaji wa MKURABITA umeanza rasmi Novemba 2004 Tanzania Bara na
Zanzibar.Azma ya Serikali ni kuwezesha watanzania wengi kushiriki katika fursa
za uchumi kupitia rasilimali na biashara zilizorasimishwa.
1.1 Lengo la Kuanzishwa MKURABITA
Lengo
la serikali kuanzisha MKURABITA ni kuwawezesha wananchi wanaomiliki rasilimali
na kuendesha biashara nje ya mfumo rasmi waweze kuzirasimisha na kuzitumia
kupata mitaji kwa ajili ya kushiriki katika uchumi wa kisasa unaondeshwa kwa
mujibu wa sheria.
M |
KURABITA
kwa kushirikiana na Mamlaka za Serikali za mitaa inatekeleza dhana ya
Uanzishwaji wa Kituo Jumuishi cha Urasimishaji,uwekezaji na Uendelezaji
Biashara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Mantiki
ya kuanzishwa MKURABITA imejengwa katika msingi wa umuhimu wa kuwawezesha
wamiliki wa rasilimali na biashara nje ya mfumo rasmi kuingia katika mfumo
rasmi. Kuingia kwao katika mfumo rasmi kutawawezesha kutumia rasilimali na
biashara zilizorasimishwa kupata na kukuza mitaji ya shughuli zao za kiuchumi.
Hali hii itachangia kupunguza umasikini wa kipato katika kaya, na hatimaye
kuchangia kuinua uchumi wa taifa kwa ujumla.
Katika kutekeleza maelekezo ya kurasimisha shughuli za Bodaboda
yaliyotolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma
na Utawala Bora Mhe. Deogratius John Ndejembi alipofanya ziara MKURABITA
Desemba 2020, Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania
(MKURABITA imeweza kukutana na mdau mmoja mmoja wa Usimamizi wa shughuli za
usafiri wa Bodaboda na Bajaji nchini. Wadau hao ni pamoja na Polisi, LATRA, Halmashauri ya Jiji la Dodoma, UMAPIDO, NMB, CRDB,
Equity na Amana Benk. Mazungumzo na mdau mmoja mmoja yamewezesha maandalizi ya
rasimu ya Mpango wa Kurasimisha biashara ya pikipiki maarufu kama bodaboda
katika jiji la Dodoma.
Lengo la Serikali ni kuwawezesha
wafanyabiashara wa Boda boda na Bajaji kuendesha shughuli zao kwa mujibu wa
Sheria na hivyo kuwezesha kuchangia uwepo wa ajira na pato la taifa kwa ujumla
wake. Kupitia biashara rasmi ya Bodaboda na Bajaji wamiliki watakuwa na uwezo wa kupata mtaji na
hivyo kufanya biashara endelevu na himilivu. Mpango wa kurasimisha shughuli za
Boda boda na Bajaji umezingatia majukumu ya msingi ya kila mdau kama
yalivyoainishwa:
2.0 MAJUKUMU
YA WADAU WA URASIMISHAJI BIASHARA YA BODABODA
Wadau katika Mpango huu ni wote wanaojihusisha na
shughuli za urasimishaji biashara ya bodaboda ikiwemo usajili, leseni, Namba ya
Utambulisho wa Mlipa Kodi na uzingativu wa usalama barabarani. Aidha, kwa kuwa
lengo kuu ni kuwezesha wamiliki kiuchumi, Taasisi za fedha ni sehemu ya wadau
muhimu. Yafuatayo
ni majukumu ya msingi ya wadau wa urasimishaji biashara Bodaboda na Bajaji:-
2.1 HALMASHAURI
YA JIJI LA DODOMA
Pamoja
na mambo mengine majukumu mahsusi katika Halmashauri ya Jiji huu ni:- Kutoa leseni kwa pikipiki za magurudumu miwili na
matatu kwa kuzingatia kanuni za leseni za usafirishaji zilizowekwa na LATRA; kufanya utambuzi na usajili wa vituo vya Bodaboda
na Bajaji na katunza na kuhuisha orodha ya bodaboda/bajaji zilizosajiliwa :
2.2 MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA (TRA)
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) wanalo jukumu kubwa la kukusanya na kusimamia mapato
nchini. Majukumu mahsusi katika mpango huu ni:- Usajili wa chombo cha moto na Usajili wa Namba ya Utambulisho wa
Mlipa Kodi (TIN), Ukusanyaji
wa kodi ya Serikali.
2.3 MAMLAKA YA UDHIBITI
WA USAFIRI ARDHINI (LATRA) – MKOA WA DODOMA
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini
wanalo jukumu kubwa la kudhibiti usafiri wa barabara. Katika Mpango huu
majukumu mahsusi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini ni pamoja na:-Kutoa leseni za kuendesha biashara ya Bodaboda na
Bajaji baada ya mmiliki kusajiliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Kutathmini
ubora wa vituo na kusajili vituo vya kupakia abiria wa Bodaboda na Bajaji kwa
kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma; Kuweka na kusimamia viwango,
masharti na gharama za huduma kwa mujibu wa sheria na Kukuza ushirikiano na
taasisi zingine za Serikali
2.4 POLISI –
KITENGO CHA USALAMA BARABARANI MKOA WA DODOMA, (MKAGUZI WA POLISI MKOA)
Kitengo cha Usalama Barabarani kina wajibu wa
kusimamia na kuhakikisha usalama wa mali na watumiaji barabara. Majukumu
mahsusi katika Mpango huu ni:- Kusimamia
usajili wa vyombo vya moto na kuvifanyia ukaguzi wa ubora ikiwemo usalama
barabarani; Kutoa leseni za udereva kwa madereva wa vyombo vya
moto ambao wamefuzu mafunzo na kuwa na Register (rejesta) kanzi data ya Vituo vya Bodaboda na Bajaji ambavyo
vimesajiliwa na vinaendeshwa kwa kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa;
2.5 TAASISI ZA KIFEDHA NI CRDB, NMB NA EQUITY NA AMANA BENKI
Taasisi
za fedha zina jukumu la msingi la kupokea na kutoa fedha kwa wateja wake.
Jukumu mahsusi la mabenki haya ambayo ni wadau wa Mpango wa urasimishaji
biashara ya Waendesha Boda boda na Bajaji ni:- Kutoa mikopo ya pikipiki na bajaji kwa walengwa wa
Mpango huu;Kuhamasisha wamiliki wa bodaboda kufungua akaunti za benki na kukopa
fedha kwa ajili ya kuendesha biashara zao; Kuwezesha na kutoa mafunzo kwa
waendesha Bodaboda na Bajaji juu ya namna bora ya usimamizi wa mikopo na kuratibu
na kusimamia maendeleo ya biashara zilizotokana na mikopo ya benki.
2.6
SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII (NSSF)
2.7 UMOJA WA MADEREVA PIKIPIKI DODOMA –
UMAPIDO
UMAPIDO
ni umoja wa
hiari ulioundwa na kusajiliwa kisheria kwa madhumuni ya kuhudumia madereva wa
pikipiki za magurudumu miwili na matatu.
Aidha UMAPIDO una muundo wa
uongozi unaoongozwa na Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina na Kamati nne (4)
ambazo ni; Kamati ya Ulinzi, Maafa, Fedha na Nidhamu: Majukumu
mahsusi ya UMAPIDO katika Mpango huu ni:- Kusajili
taarifa za madereva pikipiki pamoja na vituo. Taarifa hizi (kanzidata)
zinapatikana kwa kushirikiana na jeshi la Polisi na LATRA; Kutambua
wamiliki na waajiriwa wa pikipiki;Kupendekeza kwa LATRA usajili wa vituo vipya au
kufuta kituo vya zamani kama usalama wake ni wa mashaka na Umoja
unadhamini wanachama wake wanapotaka kukopa katika vyombo vya fedha.
3.0 UTEKELEZAJI WA
SHUGHULI ZA URASIMISHAJI BIASHARA YA BODA BODA NA BAJAJI
Shughuli za urasimishaji biashara ya
waendesha Boda boda na Bajaji zilizopangwa kutekelezwa katika Halmashauri ya
Jiji la Dodoma, zinaakisi dhana ya Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA), wenye
lengo la kuwezesha wananchi kurasimisha rasilimali na Biashara wanazomiliki na
kuzitumia kama nyenzo ya kujiongezea kipato, mitaji na kupanua wigo wa ushiriki
katika uchumi wa kisasa, unaoongozwa na sheria na kanuni za uchumi wa soko la
ushindani.
Aidha, MKURABITA kufuatia makubaliano na
kikao cha kwanza cha wadau kilichofanyika Takwimu House Dodoma mnamo tarehe 26
May,2021 ilikubaliwa kuwa MKURABITA afanye Tathmini ya Utafiti wa Msingi kwa
waendesha Boda boda na Bajaji, kuhakiki vituo vilivyosajili na kuanda na
kuhuisha kanzi data ya waendesha Boda boda na Bajaji katika Halmashauri ya jiji
la Dodoma. Zoezi la Urasimishaji Biashara ya Boda boda na Bajaji lilianza kwa
kufanya tathmini ya utafiti wa msingi kwa waendesha Boda boda na Bajaji wa jiji
la Dodoma ilianza 23/06/2021 kwa kukusanya na kufanya upembuzi wa awali na
mnamo tarehe 10 Julai, 2021ilihitimisha zoezi kwa kukusanya taarifa za
waendesha boda boda na Bajaji 2,077 kilelezo
Na.1 Kimeabatanishwa Kanzi data ya biashara ya waendesha Boda Boda na Bajaji zilizokusanywa
(baseline).
3.1
KAZI YA UWANDANI NA METHODOLOJIA ILIYOTUMIKA
Kazi
zilizopangwa ilikuwa ni Kukusanya takwimu za biashara ya waendesha Boda boda na
Bajaji kwa ajili ya Tathmini ya Utafiti wa Msingi msingi (Business baseline survey) na kuendesha mafunzo ya urasimishaji
biashara ya Boda boda na Bajaji.
Kazi
ilianza uwandani kwa lengo la kukusanya taarifa za wafanyabiashara ya Boda boda
na Bajaji 2,500 tarehe 23 Juni, 2021 hadi 10 Julai, 2021
ilifanyika kwa kukusanya Taarifa za waendesha Boda boda na Bajaji kupitia
dodoso.Takwimu za waendesha Boda boda na Bajaji zilikusanywa kwa mfumo wa
Tehama ambapo mdodosaji aliweza kuandika taarifa za biashara ya boda boda kwa
kutumia simu ya kiganjani “Smart phone”, iliyowekewa Mfumo wa kukusanya taarifa
(kobocollect program) na dodoso lilitumika
kupata taarifa za biashara.
Picha
Na.1 Picha ikionesha Mafunzo ya Wakusanya Takwimu za Boda Boda/Bajaji
Hivyo,
mbinu na njia zilizotumika kukusanya taarifa za biashara ya Boda boda ilikuwa
ni dodoso lililohifadhiwa kwenye simu, Takwimu za biashara ya Boda boda na
Bajaji zilikusanywa kwa ajili ya kubaini mahitaji na changamoto katika
kurasimisha na kuendesha biashara zao ambapo mhojiwa aliweza kutoa taarifa zake
kwa njia ya majadiliano na mhojaji aliweza kujaza dodoso hilo na kutuma moja
kwa moja kwenye server kuu, iliyokuwa
inasimamiwa na Ofisi ya MKURABITA na
baada ya taarifa kukusanywa zilichambuliwa kupitia mfumo wa “Excel Analyser”; baada ya uchambuzi,
taarifa ya matokeo imeandikwa kwa kuzingatia malengo mahsusi ya tathmini.
Picha Na 2: Mafunzo ya Mfumo kwa
Wakusanya Taarifa za Boda boda na Bajaji
Uchambuzi
wake ulilenga kupata taarifa za mahitaji halisi ya biashara ya boda boda na
Bajaji ili kuiwezesha timu ya urasimishaji kupanga vizuri mafunzo yaliyolenga
kutatua changamoto ambazo wafanyabiashara walengwa wamekuwa wakikumbana nazo
katika uendeshaji wa biashara ya Boda boda na Bajaji.
3.2
LENGO LA TATHMINI YA UTAFITI WA MSINGI KWA WAENDESHA BODA BODA NA BAJAJI JIJI
LA DODOMA
Tathmini
ya utafiti wa msingi kwa wafanyabiashara wa Boda boda na Bajaji katika
Halmashauri ya Jiji la Dodoma hutumika kubainisha aina ya mafunzo yanayotakiwa
kutolewa na Namba ya Utambulisho wa mlipa kodi, usajili wa biashara ya Boda
boda na Bajaji, leseni za udereva, leseni ya usafirishaji Piki Piki na Bajaji.
Aidha,
zoezi la tathmini ya msingi ililenga kufanyika sambamba na usajili wa biashara
ya Boda boda na bajaji katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Malengo mahsusi ya
tathmini yalikuwa Kama ifuatavyo:-
i.
Kubaini
umiliki wa biashara za Boda boda na Bajaji
ii.
Kubaini
waendesha boda boda na bajaji
iii.
Kubaini
upatikanaji wa mitaji na mauzo;
iv.
Kubaini
usajili wa biashara ya boda boda na Bajaji;
v.
Kubaini
upatikanaji wa ajira kupitia biashara ya Boda boda na Bajaji;
vi.
Kubaini
upatikanaji wa mikopo kwa wafanyabiashara wa Boda bodaa;
vii.
Kuwezesha biashara Boda boda kuwa na
mahusiano na Taasisi za kifedha ili kupata huduma zitolewazo na Taasisi hizo.
viii.
Kubaini
upatikanaji na uhitaji wa mafunzo ya urasimishaji biashara ya Boda boda
4.0 MATOKEO YA TATHMINI YA UTAFITI WA MSINGI
KWA WAENDESHA BODA BODA NA BAJAJI KATIKA HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA
Ukusanyaji
na uchambuzi wa taarifa za biashara ya waendesha Boda boda na Bajaji 2,077
ulifanyika na kufanikiwa kufanya uchambuzi na matokeo ya uchambuzi wa taarifa
umeonyesha; Matokeo kwa
kila lengo mahsusi yameelezwa katika kipengele Na. 4.1 hadi 4.6 Kama ifuatavyo:
4.1 Kubaini umiliki wa Boda boda na Bajaji
Kubaini sifa muhimu za wamiliki wa biashara
kama jinsia, umri, umiliki ni muhimu katika kuainisha mahitaji halisi ya
watumiaji wa boda/Bajaji ili kuwezesha kuandaaji wa mipango ya maendeleo.
Matokeo kwa Muhtasari ni kama yanaovyoonekana kwenye kielelezo Na. 1 na maelezo
ya kina yanachambuliwa:-
a)
Utumiaji
wa boda boda na bajaji; eneo hili lilibainishwa ili kupata hali
kiwango cha watumiaji wa bodaboda na bajaji. Matokeo yanaonesha, kati ya
watumiaji 2,077 waliofikiwa, asilimia 87 wanatumia bodaboda ikilinganoshwa na asilimia ya biashara 13 bajaji, hivyo serikali kwa
kushirikiana na wadau kutoa kipaumbele kwa kundi hili kubwa.
b)
Aina
ya Umiliki: Kubaini umiliki ni eneo muhimu ili kubaini
aina ya umiliki wa Boda boda/bajaji. Matokeo yanaonesha, kati ya watumiaji
2,077, asilimia 61 wanamiliki kwa mkataba ikilinganishwa na asilimia 39
wanaomiliki wenyewe, hivyo serikali kwa
kushirikiana na Taasisi za fedha ili kuongeza kasi ya umiliki binafsi wa Boda
boda/bajaji kwa kuwawezesha ili kumpa tija mtumiaji.
c) Jinsia;
uchambuzi wa wanawake na wanaume ni kiashiria muhimu katika kubaini mahitaji ya
kijinsi kwa waendesha Boda boda na bajaji. Matokeo yanaonesha kati ya watumiaji
2077, Wanawake ni asilimia 1
ikilinganishwa na wanaume asilimia 99.
Hali hii inaonesha wanaume ndiyo watumiaji zaidi wa Bodaboda/bajaji, hivyo
serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuongeza kasi ya uhamasishaji
kwa wanawake kushiriki na kutumia Bodaboda/bajaji kibiashara.
d)
Umri;
Uchambuzi
wa umri ni kiashiria muhimu katika kubaini mahitaji ya kwa kuzingatia umri wa
watumiaji Bodaboda na bajaji. Matokeo yanaonesha kati ya watumiaji 2, 077,
asilimia 84 wana umri kati ya miaka 18-34 ikifuatiwa na asilimia 13 wenye miaka
kati 36-44. Hali hii inaonesha uandaaji na
utekelezaji wa mipango ya maendeleo utoe kipaumbele hasa kundi la vijana.
e)
Elimu:
Uchambuzi
wa elimu umefanyika ili kubaini viwango vya uelewa ili kusaidia wakati wa
uandaaji mpango wa mafunzo. Matokeo yanaonesha kati ya watumiaji 2,077, asilimia 46 wana elimu ya msingi
ikifuatiwa na asilimia 40 wenye
elimu ya sekondari. Hali hii inaonesha uandaaji
na utekelezaji wa mipango ya maendeleo lizingatie elimu za wamiliki hasa msingi
na sekondari.
4.2 Kubaini upatikanaji wa Mitaji na Mauzo
kwa waendesha Boda/Bajaji
Upatikanaji
wa mitaji na mauzo ni eneo muhimu ili kubaini vyanzo halisi vya mitaji ya
waendesha bodboda/bajaji. Matokeo kwa Muhtasari ni kama yanaovyoonekana kwenye
kielelezo Na. 2 na maelezo ya kina yanachambuliwa baada ya kielelezo
a)
Chanzo
cha mtaji: chanzo cha Mtaji ni kiashiria muhimu katika
kubaini chanzo cha mapato kwa waendesha boda/bajaji. Matokeo yanaonesha, kati
ya watumiaji 2,077, asilimia 45 yanatokana na pesa binafsi ikifuatiwa na asilimia 43 inatokanan na mali
ya kuazima. Pia, ni asilimia 5 tu ya mitaji inatokana na taasisi za fedha. Hali
hii inaonesha, juhudi zinahitajiika kati
ya serikali na taasisi za fedha ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa mitaji
kupitia mikopo kwa waendesha
boda/bajaji. Pia matokeo yanaonesha waendesha boda wana mitaji kati ya chii ya
TZS 100,000(asilimia 40) na kati ya 100,000-500,000(asilimia 40) ikifuatiwa na
asilimia 17 wenye mitaji zaidi ya TZS 1,000,000
b)
Utunzaji
kumbukumbu: Utunzaji kumbukumbu ni muhimu ili kupata taarifa sahihi za
mapato na matumizi. Matokeo yanaonesha asilimia 52 ya waendesha boda/bajaji wanatunza
kumbukumbu ikilinganishwa na asilimia 48 wasiotunza kumbukumbu.
c)
Mapato: Kiwango cha
mauzo ni eneo muhimu ili kubaini ukubwa wa shughuli na ukuaji wake. Matokeo
yanaonesha waendesha boda/bajaji wanapata kwa siku wastani wa mauzo ya kati TZS
10,000-50,000 ikifuatiwa na asilimia 45 wanaopata chini ya TZS 10,000.
4.3 Kubaini usajili wa biashara ya
bodaboda/bajaji
Usajili wa bajaji na bodaboda ni takwa la kisheria
linalosimamiwa na Mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA). Uchambuzi
umezingatia, Usajili wa chombo, Leseni, Vituo, Bima, Matokeo kwa Muhtasari ni
kama yanaovyoonekana kwenye kielelezo Na. 3 na maelezo ya kina yanachambuliwa
baada ya kielelezo.
a)
Usajili
wa kituo; Uchambuzi wa usajili wa vituo vya bajaji/bodaboda ni
muhimu ili kupata taarifa za msingi za watumiaji wa bodaboda/bajaji. Matokeo
yanaonesha kati ya wamiliki 2,077, asilimia 64 wako katika vituo
vilivyosajiliwa kisheria ikilinganishwa na asilimia 36
hawako katika vituo vilivyosajiliwa
kiasheria. Hivyo Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa usafiri wa
boda/bajaji kuongeza juhudi ya kuhamasisha usajili wa vituo hivyo.
b)
Usajili
LATRA; Uchambuzi wa usajili wa boda/bajaji ni matakwa ya
kisheria chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (LATRA). Matokeo yanaonesha kati ya wamiliki 2,077, asilimia 83 wamesajiliwa LATRA ikilinganishwa na asilimia 17 wasio
usajiliwa. Hivyo Halmashauri imekasimiwa madaraka kwa kushirikiana na
wadau wa usafiri wa boda/bajaji kuongeza juhudi za uhamasishaji usajili wa
matumizi ya vyombo hivyo.
c)
Usajili
wa Leseni ya Udereva; Uchambuzi wa usajili wa leseni za
boda/bajaji ni hitaji la kisheria kwa watumiaji wote kuwa na leseni ya utumiaji
wa boda/bajaji. Matokeo yanaonesha kati
ya wamiliki 2,077, asilimia 76 wana leseni za udereva
ikilinganishwa na asilimia 23
wasio leseni. Hivyo
Halmashauri kwa kushirikiana na wadau kuongeza uhamasishaji kwa watumiaji wa
boda/bajaji kuwa na leseni sahihi za
udereva.
d)
Usajili
wa BIMA; Uchambuzi wa usajili wa leseni za boda/bajaji ni hitaji
la kisheria kwa watumiji wote kuwa na Bima ya chombo husika. Matokeo yanaonesha kati ya wamiliki 2,077, asilimia 84 wana Bima za bodaboda/bajaji ikilinganishwa na asilimia 16 wasio
na bima. Hivyo Jiji kwa kushirikiana na wadau wa usafiri wa boda/bajaji
kuongeza uhamasishaji kwa watumiaji wa boda/bajaji kuwa na leseni za udereva.
4.4 Kubaini upatikanaji wa ajira
kupitia bodaboda/bajaji
Upatikana wa ajira ni
manufaa kwa mtumiaji na faida kwa ujumla. Uchambuzi umezingatia umiliki wa
chombo, ajira, mikataba ya ajira na kujilipa mshahara. Matokeo kwa Muhtasari ni
kama yanaovyoonekana kwenye kielelezo Na. 4 na maelezo ya kina yanachambuliwa baada
ya kielelezo
a)
Wamiliki
wa bajaji/boda: Matokeo yanaonesha asilimia 74 ya wamiliki
wa bajaji ni wanaume ikilinganishwa na asilimia 24 ambao ni wanawake. Pia,
asilimia 2 zinamilikiwa na makampuni kama ubber
na bolt.
b)
Mikataba
ya ajira: Matokeo yanaonesha asilimia 70 ya watumiaji
waliokodishwa wana mikataba ya ajira ikilinganishwa na asilia 30 wasio na
mikataba. Matokeo pia, yanaonesha sababu za kutowapa mikataba ni kiutokana na
kufanya kazi kama ndugu (asilimia 35) ikifuatiwa na sababu ya kutojua umuhimu
wa mkataba (asilimia 30).
c)
Kujilipa
mshahara; Matokeo yanaonesha asilimia 77 ya watumiaji wanajilipa
mshahara ikilinganishwa na asilimia 23 wasiojilipa.
4.5 Kubaini upatikanaji wa mikopo ya
bodaboda/bajaji
Upatikana
wa mikopo ni fursa za kifedha wanazozipata watumiaji wa bajaji ili kuongeza
mtaji. Uchambuzi umezingatia, umiliki wa akaunti na upatikanaji wa Mkopo.
Matokeo kwa Muhtasari ni kama yanaovyoonekana kwenye kielelezo Na. 5 na maelezo
ya kina yanachambuliwa baada ya kielelezo.
a)
Akaunti za benki (A/C); Matokeo yanaonesha, kati ya wamiliki
2,077, asilimia 25 wana akaunti za
benki ikilinganishwa na asilimia 75 wasio na akaunti za benki.
b)
Uombaji mkopo; Matokeo yanaonesha asilimia 18 ya watumiaji
wameomba mkopo katika Taasisi za fedha ikilinganishwa na asilimia 82 hawajawahi
kuiomba mkopo.
c)
Kupata Mkopo; Matokeo yanaonesha asilimia 78 ya
watumiaji waliomba mkopo ndiyo waliopata ikilinganisjhwa na ikilinganishwa na
asilimia 25 hawakupata.
d)
Kiasi cha Mkopo; Matokeo yanaonesha asilimia 54 walipata
kati ya TZS 500,000-3,000,000 ikifuatiwa na asilimia 39 waliopata chini ya TZS
500,000.
4.6 Kubaini upatikanaji na uhitaji wa
mafunzo ya urasimishaji
Upatikana mafunzo kwa
waendesha boda/bajaji ni eneo muhimu ili kuongeza ujuzi katika kutekeleza
shughuli zao. Matokeo katika kielelezo Na.6 yanaonesha asilimia 87 ya watumiaji
wa boda/bajaji wanahitaji mafunzo. Matokeo pia yanaonesha mada zinazopendekezwa
ni pamoja na Usajili wa biashara zao (asilimia 53) ikifuatiwa na upatikanaji wa
mikopo (asilimia 53) pamoja na utunzaji kumbukumbu (asilimia 53)
Hatua za utekelezaji
wa zoezi la urasimishaji waendesha Boda boda na Bajaji Dodoma Jiji |
|||
Na. |
Shughuli |
Idadi ya siku |
Wahusika |
1 |
Kikao na Wadau Kujadili
Rasmu ya Mpango wa urasimishaji biashara boda boda |
1 |
LGA, Wadau na MKURABITA |
2 |
Kujenga Uelewa Kwa
LGAs, WEO, MEO na Viongozi wa Boda boda |
1 |
LGA, Wadau na
MKURABITA |
3 |
Kukusanya Taarifa za
Waendesha Boda boda na kuhakiki vituo vilivyosajiliwa |
10 |
MKURABITA,WEO,MEO,CDO |
4 |
Kuchambua Taarifa
zilizokusanywa za waendesha Boda Boda na Bajaji |
2 |
BFDO,RMO, AA, |
6 |
Mpango wa Mafunzo
endelevu kwa biashara ya Waendesha Boda Boda na Bajaji |
2 |
MKURABITA na Wadau |
7 |
Kikao cha wadau
kuwasilisha Tathimini ya Matokea ya Utafiti wa Msingi na maandalizi ya Mafunzo |
1 |
LGA, Wadau na
MKURABITA |
8 |
Mafunzo ya Urasimishaji
Biashara ya Boda boda/Bajaji |
Siku 1 x makundi 6 |
LGA, Wadau na
MKURABITA |
9 |
Usajili wa Biashara ya
Boda boda na Bajaji |
5 |
LGA, Wadau na
MKURABITA |
10 |
Uwezeshaji wa Boda
boda na Bajaji |
3 |
LGA, Wadau na
MKURABITA |
RATIBA
YA KIKAO CHA WADAU WA URASIMISHAJI NA UWEZESHAJI BIASHARA YA BODA BODA NA
BAJAJI – DODOMA JIJI, 11/08/2021
Muda |
Shughuli |
Mahali
|
Mhusika
|
11 August. 2021 |
Kuwasili kwenye ukumbi |
Takwimu House |
wote |
|
|||
04:00
– 05:00 |
· Ufunguzi
wa kikao · Kuwasili
na Utambulisho · Kusaini
Mahudhurio · Kupokea
Taarifa ya utafiti wa Msingi kwa waendesha Boda boda/Bajaji |
Takwimu House |
Maafisa
Kutoka MKURABITA |
05:00
-05:10 |
|
|
|
05:10
– 07:00 |
·
Kujadili Taarifa kwa ufupi
· Mpango wa utoaji Mafunzo · Mpango wa usajili na uwezeshaji wa Biashara ya Boda boda · Mpango wa mafunzo endelevu biashara ya Boda boda · Ufuatiliaji wa wanufaika wa Biashara ya Boda boda · Kufunga kikao |
Takwimu House |
LATRA,
Afisa biashara, TRA,NSSF,NMB,CRDB,Amana, Equity, Polisi usalama
barabarani,Umapindo |
07:00
– 08:00 |
Mapumziko ya Chakula &
kufunga |
Dodoma
|
Wote |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇