Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula akizungumza na viongozi wa kata ya Shibula wakiongozwa na Diwani wa kata hiyo Mhe Swila Dede wakati wa ukaguzi wa majengo ya madarasa ya shule mpya ya sekondari inayojengwa mtaa wa Semba Kwa ufadhilifedha za Serikali, nguvu za wananchi na mfuko wa Jimbo
Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula akizungumza na viongozi wa kata ya Buzuruga wakati wa ziara yake ya kufuatilia miradi inayotekelezwa Kwa fedha za mfuko wa Jimbo, hapa akipongeza wananchi wa Buzuruga kuchangia ujenzi wa msingi wa jengo la ghorofa tatu na Serikali.
***********************************
Watendaji wa halmashauri ya manispaa ya Ilemela wametakiwa kuhakikisha wanapata hati za maeneo ya shule mpya zote zinazojengwa katika maeneo mbali mbali ya wilaya hiyo.
Hayo yalisemwa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula wakati wa ziara yake katika kata za Shibula, Buzuruga na Bugogwa, ambayo madhumuni makubwa ni kuangalia shughuli za maendeleo zilizotekelezwa kwa fedha za mfuko wa Jimbo.
Mhe Dkt. Angeline amesema watendaji wanapokuwa na hati za umiliki wa maeneo ya shule zinapojengwa inakuwa rahisi kutambua mmiliki wa maeneo ni yupi jambo ambalo linasaidia sana katika kuepuka migogoro ya ardhi.
Aidha ameongeza kuwa katika kutatua changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu kupitia mfuko wa Jimbo kwa mwaka uliopita nguvu kubwa ilielekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu ya elimu hasa ujenzi wa shule mpya za sekondari Kwa kushirikisha nguvu za wananchi, Serikali na mfuko wa jimbo.
Akaongeza kuwa kwa mwaka huo wameelekeza katika miundombinu kwa sababu wana shule 24 za sekondari, Lakini uhitaji ni mkubwa katika hizo shule pia kuna baadhi ya kata ni kubwa na watoto wanatembea mwendo mrefu
“Tumeenda shule zote mpya tumeanzia Igogwe Kata ya Bugongwa, Semba Kata ya Shibula, Buzuruga pia Kuna Bujingwa iliyopo kata ya Buswelu, hizi zote ni shule mpya ambazo tumeelekeza ili kupunguza adha ya watoto kwenda mwendo mrefu kufata elimu,” Amesema Dkt Angeline.
Sanjari na hayo amesema lengo la ziara hiyo kwanza ilikuwa ni kuthibitisha kile nilichotoa kutoka kwenye mfuko wa Jimbo kimekwenda eneo husika na kimetumika, kujua wamefikia hatua gani ili kujua namna bora ya kuweza kukamilisha.
Lengo langu ni kuhakikisha inapofika Januari mwakani watoto waende kwenye shule hizo, ambazo zitakuwa zimewapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu.
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa Kata ya Bugogwa, Masunga Mpandachalo amesema katika ujenzi wa shule ya sekondari Bugogwa wanakabiliwa na tatizo la uchangiaji wa shule hiyo kutoka kwa wananchi kwani mwamko ni mdogo sana licha ya kukubaliana kwenye vikao husika.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Shibula, Maulina Kibwana amesema changamoto wanayokabiliwa nayo katika ujenzi wa shule mpya ya Semba wanadaiwa ela ya mafundi shilingi milioni 8 na madai ya fidia ya wananchi baada ya kutwaa eneo hilo la kujenga shule lililokuwa likimilikiwa na baadhi ya wananchi.
Hata hivyo mgawanyo wa matofali kwa mfuko wa Jimbo kwa shule za msingi,sekondari na zahanati ni 78,983.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇