LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 4, 2021

DC MWENDA ARIDHIA KUENDELEA UCHIMBAJI DHAHABU KATIKA MGODI WA SEKENKE, AAGIZA MASHARTI YA USALAMA YASINGATIWE

Na Mwandishi Maalum, Iramba

MKUU wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda ameridhia rasmi kuendelea shughuli za uchimbaji madini ya dhahabu katika mgodi wa Sekenke One uliokuwa umefungwa tangu mwaka 2019 Wilayani Iramba Mkoa wa Singida.


DC Mwenda aliridhia kurudisha uchimbaji huo wa madini juzi, wakati akizungumza katika Mkutano wake na Uongozi wa Sekenke One, Maafisa Madini wa mkoa wa Singida na Wakuu wa Idara za Serikali kutoka Halmashauri ya Iramba, uliofanyika katika eneo la Mgodi huo wa Sekenke One uliopo katika Tarafa ya Shelui, Iramba.


“Mimi ni msimamizi wa usalama wa raia na mali zao ikiwa nimehakikishiwa kuwa wachimbaji hawa watakwenda ardhini na kurudi wakiwa salama basi sina pingamizi, sasa narudisha rasmi shughuli za uchimbaji hapa.


Kwa kuzingatia thamani na umuhimu wa wachimbaji wadogo wenye mchango mkubwa nchini, tunaruhusu vijana waje hapa waendelee na shughuli za uchimbaji ambazo zitakuwa zimewapatia ajira na kutimiza mpango wa serikali. ” alisema DC Mwenda ambaye alifanya mkutano na viongzi na maafisa hao akiwa katika ziara zake za utatuzi wa kero mbalimbali kwa wananchi wa Wilaya yake.


DC Mwenda aliwataka Wajumbe wa Bodi ya Mgogi huo wa Sekenke One, kuhakikisha wanazingatia kanuni na taratibu katika uchimbaji wa duara 00 na 27 na mengine yaliokuwa salama kwa namna ya utafiti uliofanywa na wataalamu na kuionya bodi hiyo kutoyaendea maduara 12 yaliyuziwa kutokana na changamoto anuai katika eneo hilo.


Alimuagiza Kaimu Afisa Madini Mkazi kukutana na wachimbaji wadogo wadogo ili wamwandikie barua ya kujidhamini katika uchimbaji wao dhidi katika eneo hilo na wakishafanya hivyo wafunguliwe kuendelea na shughuli za uchimbaji  katika mgodi huo ambapo Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Chone Malembo alimuhakikishia Mkuu huyo wa Wilaya kuwa wachimbaji hao walikwisha andika barua hizo kwa ajili ya kuchimba katika maeneo ambayo ni salama.


Kwa upande wake  Katibu wa Bodi ya Sekenke One ambaye ni mmoja wa miliki wa mgodi huo, Joseph Mnemba aliishukuru serikali kwa kufungua mgodi huo kwa sababu maisha ya wananchi yalikua magumu, hivyo wanamuomba Mungu awasadie neema zipatikane ili kila mmoja apate kipato.


Mgodi wa Sekenke one una leseni mbili za mgodi wa Sekenke namba moja na Sekenke namba mbili ambazo zilifungwa mnamo Novemba 9, 2019 kutokana na changamoto anuai. 


Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akizungumza katika Mkutano wake na Uongozi wa Sekenke One, Maafisa Madini wa mkoa wa Singida na Wakuu wa Idara za Serikali kutoka Halmashauri ya Iramba, uliofanyika katika eneo la Mgodi huo wa Sekenke One uliopo katika Tarafa ya Shelui, Iramba.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages