LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 10, 2021

CCM Blog: MUUGUZI NA DEREVA WAPATA WAFARIKI DUNIA BAADA YA KUPTA AJALI WAKIWAHISHA MGONJWA HOSPITALI, SAME

 


Same, Kilimanjaro

Muuguzi wa Zahanati ya Kisiwani na dereva wa gari la wagonjwa, wamefariki dunia baada ya gari hilo kupoteza mwelekeo na  kupinduka na kuwakati wakimuwahisha mgonjwa Hospitali ya Wilaya ya Same.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha Agosti 8, 2021 kutokea kwa ajali hiyo Agosti 7, 2021 mda wa jana jioni katika barabara ta Same kisiwani, eneo la Majevu, Kata ya Kisima, wilayani Same.


Amewataja waliofariki dunia kuwa ni muuguzi wa zahanati hiyo, Joshua Methew (29) na dereva Jumanne Makumbe (48).


Wengine ambao wamejeruhiwa ni Ester Laizer (35), Magdalena Kuvaa (45) na Paresetwi Peutu (50).


Kamanda Maigwa amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo kupasuka tairi la nyuma na kupoteza mwelekeo kisha kupinduka.


"Gari hili lilikuwa likitokea zahanati ya Kisiwani kuelekea Hospitali ya Wilaya ya Same likiwa limebeba mgonjwa. Lilipasuka tairi la nyuma na kupoteza mwelekeo na kutoka nje ya barabara na kupinduka," amesema Kamanda Maigwa.


Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Same na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages