LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 14, 2021

VIONGOZI WA MACHIFU WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUANZA VIZURI

Chifu Soja Mwangove ampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuja na hatua nzuri za kuwafikia wananchi na kujua changamoto mbali mbali kupitia Viongozi wa Chama.
Akitoa Salaam kwa niaba ya Machifu wote wa tarafa ya Tembela, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Chief Mwangove alisema

“Kiukweli tumefarijika na mtindo huu mliokuja nao watu wa Chama Cha Mapinduzi, hatua hii mlioianza ya kuja kusikiliza kero za moja kwa moja kweli kabisa kabisa Mama amekuja na hatua nyingine na tunastahili kumpongeza sana sana.”

Chifu Soja Mwangove aliyasema hayo wakati wa Mkutano kwa Balozi shina namba 4, Tawi la Mwakwenye, Kata ya Inyala Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka.

Pamoja na mambo mengine  Chifu Mwangove amewataka Viongozi na Watendaji wa Serikali kuiga mfano huo kwani utasaidia sana kupunguza changamoto wanazokutana nazo wananchi.

Kwa upande mwingine Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Shaka alisema CCM imejipambanua kuhakikisha maendeleo endelevu kwa wananchi ambao waliwapa dhamana ya Kuongoza.



Ziara hiyo ambayo ni sehemu ya ziara ya  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo pamoja na Sekretarieti yake imeibua matumaini mapya kwa wananchi kwani Wananchi wengi walijitokeza na kuzungumzia changamoto zao mbele ya Viongozi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages