LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 3, 2021

SIMBA YACHAPWA NA YANGA 1-0 MBELE YA RAIS SAMIA, UWANJA WA MKAPA JIJINI DAR ES SALAAM, LEO

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog

Timu ya Soka ya Yanga 'Timu ya Wananchi' imedhihirisha ubabe baada ya kuchapa timy ya Simba kwa bao 1-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jiijini Dar es Salaam, kichapo hichi kikishuhudiwa na Rais Samia Suluhu Hassan Uwanani hapo. 


Shujaa aliyeifanya Yanga kuibuka kifua nbeke ni Kiungo Mkabaji Zawadi Mauya ambaye kakika ya 12 aliachia shuti kali lililomshinda Mlinda Mlango wa Simba Aishi Manula.


Hii ni mara ya pili kwa Yanga kupata ushindi mbele ya Rais wa Tanzania kwani msimu uliopita Yanga walishinda bao moja mbele ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati Dk. John Magufuli bao ambalo lilifungwa na Bernard Morrison ambaye yeye leo alikuwa Simba na leo mbele ya Rais Samia imekufa kwa bao moja bila.


Ushindi wa Yanga unaifanya Simba kushindwa kutawazwa kuwa Bingwa na sasa itabidi isubiri mechi nyingine ambapo itashuka dimbani Julai 7 katija Uwanja huo wa Mkapa kucheza na KMC.


Licha ya Yanga kupata ushindi huo dhidi ya Simba leo, inabaki nafasi ya pili kwa kufikisha Pointi 70 huku Simba ikibaki na pointi 73 na Mechi nne mkononi na Yanga wamebakiza mbili.


Kwa sasa macho na masikio ya Watani wa Jadi na mashabiki wao ni Julai 25, 2021 Watani hao watakapokutana tena uso kwa uso katika mechi ya fainali ya Kombe la Azam Sport Federation maarufu kama FA Cup katika  Uwanja wa Lake Tangayika mjini Kigoma.

Bao likiwa limetinga golini mwa Simba.

Rais Samia Suluhu Hassan akiishuhudia mechi hiyo ya Yanga na Simba, leo

Mshambuliaji wa Yanga Yacouba Songne akiipangua ngome ya Simba mbele ya Beki Onyango na Tshabalala katika mechi ya kibabe iliyooigwa leo katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam, na Yanga kuibuka kideedeo kwa kuifunga Simba 1-0 katija mechi hiyo ambayo imeshudiwa na Rais Samia Suluhu Hassa.

Wachezaji wa Yanga wakifurahia kupachika bao.

Mashabiki wa Timu ya Wananchi Yanga wakishangilia timu yao kupata bao dhidi ya Simba.

©CCM Blog 2021

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages