Watumishi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wameaswa kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu na kwa misingi ya uwajibikaji ili kutoa huduma bora kwa wadau wake.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Tixon Nzunda alipotembelea ofisi za Mfuko kwa ajili
ya kufuatilia shughuli zinazofanywa na WCF.
“Nimefanikiwa
kuzungumza na watendaji wa idara na vitengo vyote na moja ya maelekezo yangu ni
kuwahimiza kutoa huduma kwa umma kwa kuzingatia misingi ya ueledi, uwajibikaji
na usikivu na kuzingatia misingi na miongozo ya uendeshaji kazi serikalini”,
alisema Bw. Nzunda.
“Pia
nawasisitiza kuhakikisha kuwa utendaji wa shughuli za umma unazingatia misingi
ya kujenga ustawi wa wananchi. Tumieni rasimilimali zilizopo kwa kuzingatia
thamani ya fedha na uwekezaji ufanyike katika maeneo yenye tija ili kulinda
amali za fidia kwa wanachama”.
Bw.
Nzunda ameelekeza Mfuko kuhakikisha unaimarisha zaidi mifumo ya kielektroniki
kutoka asilimia 80 hadi 100 ili huduma zote za madai ya fidia zifanyike kwa
njia ya kielektroniki.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma, amesema Mfuko utazingatia kuimarisha huduma za kielektroniki ambapo pia unaendelea kuutangazia umma kuhusu punguzo la Tozo ya michango lililofanywa na Serikali kwa sekta binafsi kutoka asilimia 1.0 hadi 0.6. Aidha, Dkt. Mduma ameishukuru Serikali kwa hatua hiyo muhimu na kuwasisitiza waajiri sekta binafsi kuzingatia mabadiliko husika.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇