LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 23, 2021

RC MTAKA AONGOZA MKUTANOKAZI WA MKAKATI WA KUINUA MAENDELEO MKOA WA DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka akiongoza mkutanokazi wa kujadili jinsi ya kuukwamua mkoa huo kiuchumi pamoja na mambo mengine. Mkutanokazi huo umefanyika leo kwenye Ukumbi wa Informatic Chuo Kikuu cha Dodoma.
Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai akizungumza wakati wa mkutanokazi huo.
Meya wa Jiji la Dodoma, Davis Mwanfupe akizungumza wakati wa mkutakazi huo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatma Maganga akifafanua jambo wakati wa mkutanokazi huo.
Viongozi mbalimbali kutoka wilaya mbalimbali za mkoa huo wakihudhuria mkutanokazi huo ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka.


RC Mtaka akisisitiza jambo wakati wa mkutanokazi huo ambao kauli mbiu yake ni Dodoma Tunayoitaka Inawezekana. Tushirikiane kwa Pamoaja Kuitengeneza.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi,


Mbunge wa Chemba, Mohamed Monni akichangia hoja wakati wa mkutano huo.
Viongozi wa Kamati ya Siasa ya Mkoa huo wakifuatilia mkutano huo.
viongozi mbalimbali wakifuatilia majadiliano ya mkutanokazi huo.





Viongozi kutoka Halmashauri ya Wilaya Chemba wakiwa katika mkutanokazi huo.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

 

Na Richard Mwaikenda, Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka ameongoza Mkutanokazi wa kujadili mikakati ya kuinua maendeleo ya mkoa huo.

Mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai uliwashirika pia viongozi mbalimbali wa mkoa huo, wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wabunge,Meya wa Jiji la Dodoma, madiwani, Kamati za siasa na maafisa kutoka mkoani na halmashauri mbalimbali.

Mkutano umefanyika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wa Informatic ambapo wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo Hoja za CAG za Mamlaka ya Serikali za Mitaa 2019/20, Taarifa ya Mapato ya Halmashauri 2020/21 na Makisio ya 2021/22.

Pia wamejadili kuhusu maendeleo ya zao la alizeti Mkoa wa Dodoma, kuikijanisha Dodoma, kuvutia na kuongeza uwekezaji katika mkoa huo, maendeleo ya elimu, hali ya utoaji wa huduma za afya, miradi ya maendeleo iliyotekelezwa Mwaka 2020/21 na utatuzi wa migogoro ya ardhi. 


 
Kauli mbiu ya mkakati huo ni; Dodoma Tunayoitaka Inawezekana. Tushirikiane kwa Pamoaja Kuitengeneza.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages