- Ahaidi Wafanyabiashara kuwa atatumia ushawishi fedha zipatikane na uboreshaji utaanza wiki hii.
- Uboreshaji utakaofanyika ni Ujenzi wa Paa la Kivuli kwa Wafanyabiashara wahanga wa Kariakoo Shimoni waliokuwa wakiuza mbogamboga na matunda.
- Soko la Kisutu aelekeza waliopewa maeneo ya kujenga Fremu waruhusiwe kujenga na wasizungushwe na gharama zao ziwekwe wazi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ametembelea Soko la Kariakoo, Kisutu na Machinga Complex walipohamishiwa Wahanga wa Moto Soko la Kariakoo kwa lengo la kujionea Kama Kuna Changamoto ili Serikali iweze kuzitatua na Wafanyabiashara wafanye biashara zao bila usumbufu.
Akizungumza na Wafanyabiashara hao, RC Makalla amefurahi kuona wengi wao wamepata Maeneo ya kufanya biashara na wanaendelea na biashara zao Kama kawaida.
Kuhusu suala la wateja, RC Makalla ameahidi kuwa Mstari wa mbele Katika kuwatafutia wateja huku akisisitiza agizo lake la kutaka wasitozwe Ushuru kwa Muda wa miezi miwili Kama sehemu ya kifuta machozi.
Akiwa soko la Machinga Complex, RC Makalla amepokea changamoto ya kukosekana kwa Paa la kuzuia Jua na Mvua ambapo ameahidi kutafuta kiasi Cha Shilingi Milioni 62 ya Ujenzi wa Paa la Kisasa.
Pamoja na hayo RC Makalla ameelekeza Halmashauri ya Jiji la Ilala kuwaondoa Wafanyabiashara wanaoendesha biashara zao kwenye hifadhi za Barabara na kuwatafutia vizimba ndani ya Masoko hayo.
Kwa upande wao Wafanyabiashara wahanga wa Moto Soko la Kariakoo akiwemo Radhid Mohamed ameishukuru Serikali na Viongozi wa Mkoa huo kwa ushirikiano mzuri waliowapatia na licha ya changamoto waliyoipata wamempatia RC Makalla zawadi ya Viungo vya Chakula Kama sehemu ya furaha kwa Mambo mazuri Serikali iliyowafanyia.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇