LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 26, 2021

RAIS WA UFILIPINO ANATARAJIA KUTOA HUTUBA YAKE YA MWISHO YA KITAIFA

   Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte anatarajiwa kutoa hotuba yake ya mwisho ya kitaifa mbele ya bunge la nchi hiyo, akiwa anaelekea kumaliza muhula wake wa miaka sita.

Duterte anakamilisha muhula wake katikati ya janga la virusi vya corona, uchumi wa nchi yake ukiwa katika hali mbaya, na uongozi wake ukiwa umetawaliwa na malalamiko ya umwagaji damu kwa kisingizio cha vita vya kupambana na madawa ya kulevya.

 Hata hivyo, washirika wake wanaunga mkono wito wa chama tawala unaomtaka Duterte mwenye miaka 76 kugombea wadhifa wa makamu wa rais wakati muhula wake utakapoisha mnamo mwezi Juni mwakani. 

Wanasheria wa upinzani wanatishia kuipinga hatua iyo kwenye Mahakama Kuu. Aidha kuna uwezekano kwamba binti yake, ambaye sasa ni meya wa jiji la Manila, kugombea urais katika uchaguzi wa Mei 9.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages