LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 23, 2021

PINDA AKAGUA MABANDA YA WADAU NA WANUFAIKA WIKI YA MAONESHO YA TAASISI YA PASS TRUST DODOMA

Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda (katikati)  akizungumza alipotembelea banda lka Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), wakati wa Maonesho ya Wiki PASS Trust katika viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma. Taasisi hiyo inawanufaisha wakulima kupata mikopo ya  pembejeo bila dhamana kwa kuwaunganisha na  taasisi za kifedha zipatazo 14. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Anna Shanalingigwa, na Mwenyekiti wa Bodi ya PASS Trust, Dkt Taus Kida. Kushoto ni Askari wa Uhifadhi Daraja la Pili, Agnes Richard. Pass imeanzisha Kilimo Utalii ambapo mkulima ambaye ameandaa vizuri shamba lake  watu watakuwa  wanatembelea shamba kwa malipo.


Moja ya malengo ya Wiki hiyo ya Pass Trust ni kuwaunganisha wateja wao, kutatua changamoto ya upatikanaji wa mikopo, kutengeneza Networking pamoja na kujuana. Pia wamezindua Kampuni ya PASS Leasing itakayojihusisha na ukopeshaji wa zana za kilimo bila dhamana. 


Mzee Pinda akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Agricom inayouza na kukopesha PowerTiller.

Waziri Mkuu mstaafu, Pinda akiendelea kutembelea mabanda ya wanufaika wa Pass Trust kwenye viwanja vya Nyerere Square ambapo wiki hiyo itaendelea hadi kesho.







 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages