Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua cha Nextgen Solawazi LTD Lakhan Gupta, alipotembelea Kituo hicho kilichopo Mkoani Kigoma
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato akiangalia paneli zinazotumika kuzalisha umeme wa jua.
Paneli hizo zinatumika kubadilisha mwanga wa jua kwenda kwenye umeme.
Kushoto kwa Naibu Waziri Byabato, ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji Umeme TANESCO Mha. Isaac Chanji, (na kulia kwa Naibu Waziri Byabato) ni Meneja wa kituo cha Nextgen Solawazi LTD Lakhan Gupta, na Mkurugenzi Mkuu REA Mha. Amos Maganga.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato akipata maelezo kuhusu utendaji wa kituo cha Nextgen Solawazi LTD kutoka kwa Meneja wa kituo hicho Lakhan Gupta
Paneli zinatumika kubadilisha mwanga wa jua kwenda kwenye umeme.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato akizungumza na Meneja wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua cha Nextgen Solawazi LTD Lakhan Gupta, alipokitembelea kituo.hicho kilichopo mkoani Kigoma tarehe 16 Julai, 2021.
Wa tatu kutoka kulia kwa Naibu Waziri Byabato, ni Mkurugenzi Mkuu REA, Mha. Amos Maganga, anayefuatia ni Kaimu Mkurugenzi wa Umeme na Nishati jadidifu Edward Ishengoma, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji Umeme TANESCO, Mha. Isaac Chanji, pamoja na watumishi wengine wa TANESCO na REA.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO na REA alipokitembelea kituo hicho cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua cha Nextgen Solawazi LTD kilichopo mkoani Kigoma
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili kwenye kituo cha Nextgen Solawazi LTD kilichopo mkoani Kigoma
…………………………………………………………………………..
Na Dorina Makaya – Kigoma.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato amesema, Wizara ya Nishati itashirikiana na kumsimamia mwekezaji wa kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua cha Nextgen Solawazi LTD kilichopo Mkoani Kigoma ili kuhakikisha anafikisha uzalishaji wa 5MW kama ilivyokubalika kwenye mkataba uliosainiwa.
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Wakili Stephen Byabato ameyasema hayo tarehe 16 Julai, 2021 alipotembelea kituo hicho cha kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua cha Nextgen Solawazi LTD
Kituo hicho kina uwezo wa kuzalisha umeme 4MW
Hivi sasa Kituo hicho kinazalisha umeme 1.8 MW. zinazopelekwa kwenye kituo cha umeme cha TANESCO mkoa wa Kigoma.
Naibu Waziri wa Nishati amempongeza mmikiki wa kituo hicho kwa hatua aliyofikia na kuahidi kuwa Wizara ya Nishati itashirikiana na mwekezaji huyo ili kuhakikisha anafikisha uzalishaji wa 5MW kama ilivyokubalika kwenye mkataba uliosainiwa.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Byabato aliambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Umeme na Nishati Jadidifu Edward Ishengoma, Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji Umeme TANESCO, Mha. Isaac Chanji, Mkurugenzi Mkuu REA Mha. Amos Maganga, Meneja Mwandamizi Kanda ya Magharibi Mha. Sana Idindili, Meneja wa TANESCO mkoa wa Kigoma Jaffari Mpina, na baadhi ya watumishi wa TANESCO na REA.
Tanzania ni nchi mojawapo inayoweza kunufaika na vituo vya kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za mwanga wa jua kwa sababu inapata mwanga wa jua kwa kipindi kirefu katika mwaka.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇