Mkurugenzi wa Simba Cargo Jack Wang aipongeza MOI kwa jitihada za kuokoa maisha ya watu na kuwapati Tiba mbalimbali Wananchi wanaojitokeza kwenye upataji huduma,
aliyasema hayo baada ya kutembele Banda la Taasisi hiyo akiongozana na Timu yake iliyofika kwenye Banda lililopo Viwanja vya Sabasaba Julai 7, 2021 na kujionea jinsi watendaji walivyojipanga katika banda hilo na aliendelea kusema
Mimi na Timu yangu tunapenda kuwapongeza watendaji wote wa Taasisi ya MOI na wakiongozwa na Mkurugenzi wao Dkt. Respicious Boniface. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Daktari wa Taasisi ya Mifupa MOI Dr. Eugen Sebastian akiwaonesha wananchi kiungo cha mkono bandia jinsi kinachoweza saidia mtu alipatwa na tatizo la kukatika mkono.
Dkt. Taasisi ya Mifupa MOI, Dr. Isangya Lameck akimchukuwa kipimo mwananchi aliyejitokeza Bandani hapo.
Wananchi wavutiwa na Banda la Tiba Lishe lililopo katika viwanja vya Sabasaba Maonesho ya 45 Barabara ya Kilwa, wajitokeza kwa wingi Banda la Rombo One Mix Species Coffee Kutoka Manyara ambao wanatoa huduma mbalimbali ya Tiba Lishe.
Dkt. Bingwa wa Taasisi ya Mifupa MOI, Dr. Allen kisanga akionesha wananchi jinsi mivunjiko inavyotokea kwenye mfupa wa paja na matibabu yake.
Wafanyakazi wa Simba Cargo walivyoliteka Banda la MOI huku wakifurahishwa na huduma ya kwanza waliyojione Bandani hapo.
Mtaalam wa Mionzi Taasisi ya Mifupa MOI Jane Panje (wa nne kulia) akiwaonesha baadhi ya wafanyakazi wa Simba Cargo jinsi mfupa wa paja unavyo fanya kazi pale mtu anapopatwa na tatizo hilo mara walipolitembelea Banda la Taasisi hiyo.
Afisa Muunguzi na Msimamizi chumba cha cha Upasuaji Taasisi ya Mifupa MOI Juma Rehani (wa kwanza kulia) akiwaonesha mfano wa mgongo mara mtu anapo jiona na dalili katika eneo hilo na kuwa na tatizo kwenye pingili za mgongo na nini afanye kwa hatua yakwanza.
Wafanyakazi Taasisi ya Mifupa MOI wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Simba Cargo mara walipo fika katika Banda hilo.
Mkuu wa Kitengo Viungo Bandia Geoffrey Mwakasungula (kulia) akiwaonesha wananchi mfano wa mkono bandia kwa mtu mwenye tatizo hilo jinsi unavyo weza kumsaidia kufanya shughuli zake.
Afisa Mfiziotherapia Emmanuel Jacob akimfanyia mazoezi mtoto aliyefika na mama yake Bandani hapo.
Dkt. Isangya Lameck ampatia huduma bila malipo mama aliyejitokeza katika Maonesho ya 45 na kufika Bada la MOI Viwanja vya Sabasaba Barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salam.
Afisa Mfiziotherapia Emmanuel Jacob akimfanyia mazoezi mwananchi aliye fika Bandani kujiptia huduma.
Mwananchi akiwa katika pozi mara alipotembelea Banda la Taasisi ya Mifupa MOI. Kulia ni mwanaye aliyeongozana naye.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇