LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jul 12, 2021

MAJALIWA AIPA SIKU SABA TUME KUCHUNGUZA CHANZO CHA MOTO SOKO LA KARIAKOO

  

 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua hatua zinazoendelea kuchukuliwa kudhibiti moto uliyotokea kwenye soko la Kimataifa la Kariakoo

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala, wakati akikagua hatua zinazoendelea kuchukuliwa kudhibiti moto uliyotokea kwenye soko la Kimataifa la Kariakoo

  

Muonekano wa Soko la Kimataifa la Kariakoo baada ya kuungua usiku wa kuamkia 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiongea na Wafanyabiashara wa Soko la Kimataifa la Kariakoo, baada ya kukagua hatua zinazoendelea kuchukuliwa kudhibiti moto uliyotokea kwenye soko la Kimataifa la Kariako

Wafanyabiashara wa Soko la Kimataifa la Kariakoo, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, baada ya kukagua hatua zinazoendelea kuchukuliwa kudhibiti moto uliyotokea kwenye soko la Kimataifa la Kariakoo, Julai 11, 2021.

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

.

Waziri Mkuu Kaasim Majaliwa ameipa siku saba za awali tume aliyoiunda kuchunguza chanzo cha moto katika soko la kimataifa la Kariakoo ili kubaini nini kimesababisha au nani kasababisha moto huo.

Ametoa kauli  (Jumapili Julai 11, 2021) alipokuwa anaongea na wafanyabiashara na wakazi wa eneo la Kariakoo baada ya kukagua hatua zinazoendela kuchukuliwa kudhibiti moto huo, Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa kamati iliyoundwa ambayo itafanya kazi na kamati ya ulinzi na usalama iliyoanza kufanya kazi chini ya Mkuu wa Mkoa huo itajumuisha Ofisi ya Rais-Ikulu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo itawakilishwa na Mkurugenzi wa Maafa.

Wengine ni Vyombo vya Ulinzi na Usalama ikujumuisha Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi, Zimamoto pamoja na Taasisi ya Kupambana na Rushwa. Pia Waziri Mkuu alizitaja Wakala wa Majengo, Shirika la Umeme (TANESCO), Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP)

“ Endapo itagundulika kama kuna mtu alihusika kwa namna moja au nyingine, hatua kali za kisheria zitachukuliwa moja kwa moja, kitendo cha kuungua kwa soko hili la miaka chungu mzima lazima kuwe na uchunguzi wa kina, kwanini leo lishike moto”

Aidha, Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara katika soko hilo wawe watulivu wakati Serikali inafanya kazi yake ya kujua chanzo cha moto huo na amewahakikishia usalama wa mali zilizo ndani ya soko hilo

Waziri Mkuu pia aliwataka wafanyabiashara kutoingia ndani ya soko hilo katika kipindi hiki ambacho udhibiti unaendelea hadi pale timu zilizoundwa zitakapojiridhisha na utulivu na kufanya sensa ya watu wenye mali kuingia mmoja baada ya mwingine ili wakatoe vitu walivyoviacha

“Tunachoshukuru kule chini shimoni hakuna moto, mali zote zinalindwa, msiwe na mashaka milango yote imefungwa na makamanda wako ndani na nje wanalinda, mali zote zimehifadhiwa, msiwe na mashaka”

Kadhalika Waziri Mkuu amewaahidi wafanyabiashara hao kuwa Serikali itaongea na Mabenki yaliyowakopesha wafanyabiashara waliounguliwa na mali zao kuwaongezea muda wa kulipa mikopo yao baada ya kuunguliwa.

“Tume itapata taarifa za kila mmoja mwenye mkopo rasmi kwenye taasisi za fedha ili tuzungumze nao waongeze muda waache kipindi hiki ili uweze kulipa hapo baadae utakapo kuwa umetulia,biashara imeungua naamini mabenki yatatuelewa na kuweka utaratibu mzuri”

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages