Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Abubakar Kunenge amefanya ziara ya Kampeni ya Kutokomeza Migogoro ya Ardhi ,Wilaya ya Kibaha huku akiwa ameambatana na William Lukuvi, Waziri wa Ardhi.
Wakiwa katika Eneo lenye Mgogoro wa Ardhi, la Wananchi Kuvamia Eneo la DIMARA Agriculture Cooperative Ltd, Mlandizi Kibaha,
Wanachi hao wamekiri kuwa wamevamia eneo hilo kutokana na makazi yao kukubwa na mafuriko mwaka 2012.
Lukuvi, ameeleza kuvamia maeneo ya watu ni sawa na Ujambazi na kuongezwa kuwa yupo kuwalinda watu wote waliomilikishwa Ardhi Kisheria.
Akitoa Maelekezo kwa Wavamizi hao Lukuvi amewapa eneo la Makazi katika Ekari 51 zilizofutwa na Rais na kuwataka waondoke mara moja eneo hilo.
Ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya kibaha Kushirikiana na mwenye eneo kupanga Mji kwenye eneo hilo.
Nae Kunenge amewataka Wanachi kuheshimu Sheria na kuacha kuvamia maeneo yanayomilikiwa kihalali, na kama ni suala la mafuriko wangeomba Serikali iwasaidie.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇