Kuna maajabu ambayo wataalam wa maendeleo wanayaita Phenomenon! kila Bara, Kaskazini ni matajiri na Kusini ni maskini.
Kwa mujibu wa Kitabu cha Mwanzo 27:27-40, Baraka huwa ni Moja; Shamba ni Moja; Bustani ni Moja; Moyo ni mmoja na zaidi ya yote, CHANZO CHA MEMA NA MAZURI, yaani MUNGU BABA ni Mmoja.
Wote tukifahamu hayo, ugomvi na vita kila mahali itakuwa hakuna.
Katika Mwanzo 25:24-26, Yakobo na Esau walizaliwa wakiwa mapacha kutoka katika Tumbo Moja. Yakobo alikuwa wa pili kuzaliwa, ni Mweusi alikuja Kusini. Esau alikuwa wa kwanza kuzaliwa, alienda Kaskazini.
Yakobo, aliyekuja Kusini, mahali ambapo katika kila Bara ni maskini, ndiye aliyekuwa wa kwanza kubarikiwa kwa kupewa yaliyo manono ya nchi, mazuri ya umande wa Mbingu, na kwamba kila atakayemlaani alaaniwe na kila atakayembariki abarikiwe.
Esau, alipewa Baraka kama hizo alizopewa Yakobo, lakini yeye aliambiwa atazipata kwa upanga! Yote haya ni kwa mujibu wa Mwa.27:27-40.
Esau, baada ya kuona amepewa Baraka lakini kwa Upanga, alitafuta mbadala wa kupata Baraka hizo kutoka kwenye shamba lile lile, bustani ile ile, moyo ule ule. Mbadala huo wa kupata baraka tunausoma katika Matendo ya Mitume 20:35.
Esau aliposoma katika Matendo ya Mitume 20:35, alikuta imeandikwa kuwa “ni Heri kutoa kuliko kupokea”.
Hivyo, Esau akajua Heri ni sawasawa na ile Baraka ambayo hakuipata moja kwa moja. Aliamua kujikita katika kutoa misaada na mikopo ndio ukawa upanga wake.
Yakobo, kwa kuwa alipewa kila kitu alijikuta ni mvivu wa kutoa. Katika kitabu cha Warumi 2:9-10, Esau alikuta mahali palipoandikwa kuwa, anayependa kutoa anapata Amani, Heshima na Utukufu.
Asiyependa kutoa atapata dhiki na shida.
Esau, aliposoma tena katika Wafilipi 4:16-19, akagundua kuwa Yakobo amekataa kumtunza Mtume Paulo, ndipo Esau akaamua kumtunza Paulo. Mtume Paulo katika Wafilipi 4:19 akamtamkia Esau kuwa apate kila anachokihitaji kwa kadri ya utajiri wa MUNGU wa Majira Saba.
Ndicho kilichotokea kwa Esau. Kwa kuwa Yakobo hakutenda mema, yeye akapata dhiki na shida katika majira hizo saba.
MUNGU BABA ambaye ni CHANZO HALISI CHA MEMA NA MAZURI amekuja, kwa mujibu wa 1Wakorintho 15:24-28, amekuta watoto wawili ambao ni Yakobo na Esau, mmoja anapenda kutoa na amepata Amani, heshima na utukufu, ila kwa mujibu wa Mwanzo 27:27-40 hakupata Baraka.
Yakobo, yeye alibarikiwa ila hapendi kutoa, matokeo yake akajikuta amepata dhiki na shida! Yakobo ndiye amepata upendeleo wa kumpokea MUNGU BABA ambaye ni CHANZO CHA MEMA NA MAZURI, ila hapendi kutoa na ana dhiki na shida.
Esau ambaye hakubarikiwa kwa mujibu wa Mwanzo 27:27-40, MUNGU BABA hakushukia kwake. Kwa mujibu wa Waefeso 4:4-6, huyu MUNGU BABA aliye CHANZO CHA MEMA NA MAZURI anawapenda Yakobo na Esau. Kitu gani afanye?
Jibu sahihi ni kugeuza misaada na mikopo kutoka kwa Esau iwe shukrani kwa MUNGU BABA, ili Yakobo na Esau wote sasa wapate Baraka kutoka kwa Aliye Chanzo cha Baraka.
Yakobo (Kusini) anaye CHANZO CHA MEMA NA MAZURI ila hapendi kutoa. Esau (Kaskazini) hana CHANZO CHA MEMA NA MAZURI ila anapenda kutoa. Ili MUNGU BABA Aliye CHANZO CHA MEMA NA MAZURI, ahudumie wote (Efeso 4:4-6), ilikuwa ni lazima amalize ugomvi na vita kati ya hawa wawili kwa kugeuza misaada na mikopo kutoka kwa Esau kuwa shukrani kwake.
Sasa Yakobo (Kusini) hadaiwi tena maana ule upanga aliopewa Esau haupo. Wote wawili wanapata kutoka kwa MUNGU BABA–CHANZO HALISI.
Hili halikwepeki maana hata Musa alioa Afrika (Hesabu 12:2-8). Yesu baada ya kuzaliwa, alihifadhiwa Afrika ili apone (Mathayo 2:1-15). Yesu pia wakati wa kubebeshwa msalaba alisaidiwa na Afrika (Marko 15:21 na Luka 23:26).
Lakini pia Majira sahihi imerejeshwa na aliyetoka Mashariki Halisi (Tanzania –Afrika) katika Isaya 41:2,4. Kwa kuwa huwezi kufanya chochote bila Majira, basi Esau na Yakobo wote wanamhitaji huyu MUNGU BABA aliye CHANZO HALISI CHA MEMA NA MAZURI. ndiyo maana ilikuwa ni lazima kusawazisha ili Esau na Yakobo wasigombane tena.
Hii ina maana kuwa misaada na mikopo ambayo Afrika iliwahi kupata kwa Esau haidaiwi tena. Heri uliyebarikiwa kuliko wote.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇