Na Richard Mwaikenda, CCM Blog, Dodoma
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula amefungua kikao kazi cha wakaguzi wa ndani na wahasibu wa wizara hiyo na taasisi zake sita cha kuweka uelewa wa pamoja wa kujibu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kabla ya kufanyiwa ukaguzi.
Kikao kazi hicho kimefanyika leo katika Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dodoma.
"Tumeamua leo tukae pamoja tupeane ABC tuwe na mipango ya bajeti , mipango lazima iakisi uhalisia wa matumizi yake na mambo tunayotarajia kuyafanya, mwaka jana tulikuwa kidogo vizuri na mambo ambayo hatukuyafanya vizuri katika baadhi ya taasisi kwa sababu kulikuwa na sitofahamumambo ambayo tulikuwa bado hatujayafahamu vizuri tujue tatizo ni nini na changamoto nini,"amesema Dkt Chaula.
Dkt. Chaula amewataka wakaguzi wa ndani na wahasibu wa taasisi zilizochini ya wizara hiyo kuhakikisha wanafanyia kazi hoja zote zilizojitokeza katika ripoti ya CAG na kuhakikisha hoja hizo hazijirudii tena na hatarajii kuona makosa tena katika ripoti ya CAG.
Aidha dakta chaula amewasisitiza wataalamu hao kuhakikisha wanawekeza katika matumizi ya tehama katika majukumu yao ili kufikia malengo malengo waliyojiwekea.
Naye Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa wizara hiyo, CPA Joyce Christopher amesema lengo la kuwakutanisha wahasibu na wakaguzi ni kuweka uelewa wa pamoja na kuwapa maelekezo ya namna bora ya kufunga mahesebu yao ya mwisho kuepuka kasoro kwenye ripoti ya CAG.
Mkaguzi wa ndani wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), CPA Octaviani barbanas amemshukuru Katibu Mkuu Dkt. Chaula kwa kukiandaaasema kikao hicho cha wataalamu wa ukaguzi na uhasimu na kwamba kimewawasaidia kubadilishana uwezo.
.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇